Ridhiwani aipa tano Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, ameipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa mageuzi makubwa iliyofanya katika mashirika ya umma.

Kikwete ametoa pongezi hizo leo Julai 4, 2025, alipotembelea banda namba 39 (Ukumbi wa Kilimanjaro) katika maonesho ya 49 ya biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

“Tunaishukuru Ofisi ya Msajili wa Hazina chini ya uongozi imara wa Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, kwa kuwezesha taasisi za umma kuongeza ufanisi wao,” amesema Kikwete.

Ameongeza: “Wote ni mashahidi, katika uongozi wa awamu ya sita chini ya Mhe. Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika taasisi za umma.

”Ofisi ya Msajili wa Hazina imewezesha kuimarika kifedha kwa mashirika ya umma yaliyokuwa na mitaji hasi na yaliyokuwa yanapata hasara mfululizo, ambapo sasa yameweza kuondokana na utegemezi wa ruzuku ya Serikali na kufanikiwa kutoa gawio.

Baadhi ya mashirika hayo ni pamoja na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ambapo mchango wake katika Mfuko Mkuu wa Serikali ulikuwa Sh10.5 bilioni katika mwaka wa fedha 2024/25.

Pia, katika orodha ya mashirika ambayo kwa sasa yanajiendesha kwa ufanisi ni Shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Shirika la Umeme (TANESCO), na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhe. Kikwete alisema serikali itaendelea kuiunga mkono ofisi ya Msajili wa Hazina katika kuhakikisha safari ya mageuzi inafanikiwa.

“Endeleeni kufanya kazi kwa bidii na pale ambapo kuna mambo mnataka yabadilike katika taasisi ambazo ziko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hesabuni mmepata ushirikiano kutoka kwetu,” alisema amesema Kikwete.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la ufanisi kwenye baadhi ya Mashirika kutokana na mageuzi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika katika Mashirika ya umma.

“Ufanisi umeimarika kwa kiasi kikubwa, mfano mzuri tunauona kwenye Mamlaka ya Bandari,” amesema Kosuri.

Kwa mwaka huu wa fedha uliopita, pamoja na kuongeza mchango kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kutoka Sh155.7 bilioni mwaka 2023/24 hadi Sh181 bilioni mwaka 2024/25, matumizi ya kawaida kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa bandari pia yamepungua kwa kiasi cha Sh505.59 bilioni sawa na ufanisi wa asilimia 46.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...