TMDA yaendelea kuelimisha umma juu ya matumizi sahihi ya dawa Sabasaba

Na Tatu Mohamed

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Imeendelea kutoa Elimu kwa Umma juu ya matumizi sahihi ya Dawa na vitenganishi ndani ya maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara (SabaSaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Temeke, Dar Es Salaam.

Akizungumza katika banda la Stone town ndani ya maonesho hayo ya Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo amesema kama Mamlaka mara kwa mara wataendelea kutoa elimu kwa Umma ili kusaidia Jamii kuwa na uelewa wa matumizi sahihi ya Dawa.

Amesema majukumu makubwa ya TMDA ni kusajili dawa za ndani na zinazotoka nje kuingia nchini hii ni pamoja na kufanya ukaguzi kila siku ikiwemo kwenye maduka ya Dawa, masoko na mipaka ili kumlinda mtanzania.

“Sisi jukumu letu kuhakikisha kwamba dawa inatumika kama ilivyokusudiwa na sio kumdhuru mtumiaji.Majukumu yetu ni kuhakikisha tunasajili dawa zilizosajiliwa na kukidhi soko la nchi yote hii ni kumlinda Mtanzania katika usalama wa dawa hivyo tunahakika ubora na ufanisi.

“Vile vile tunafanya kazi tunapima bidhaa za dawa kupitia Maabara zetu za kisasa ambazo zina ubora wa Kimataifa wa WHO,” amesema Dkt. Adam Fimbo.

Aidha, katika banda hilo la TMDA, Dkt Adam Fimbo ametoa elimu kwa Wananchi waliotembelea juu ya matumizi sahihi ya Dawa na kuacha kutumia bidhaa hiyo kiholela bila kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu ili kuepuka usugu wa dawa.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this