TRA yawaalika wananchi Sabasaba kupata elimu ya Kodi na huduma za TIN

Na Tatu Mohamed

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imewaita wananchi kutembea banda lao lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba ili kupata elimu na huduma mbalimbali za kikodi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika Viwanja vya Maonesho hayo ambayo ni ya 49, Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi na Mawasiliano wa TRA, Richard Kayombo amesema wameshiriki katika Maonesho hayo kwa ajili ya kuendeleza kutoa elimu ya kodi kwa wadau wanaofika katika viwanja hivyo.

Amefafanua kuwa katika maonesho hayo TRA ina mambo mengi ikiwemo kuwaelekeza watu kuagiza bidhaa pamoja kuwaelekeza bidhaa zenye misamaha ya kodi.

“Tumeona tuje ili kuwaelimsiha wadau mambo mapya na ya zamani kuhusu Chuo cha kodi, vivutio vya kodi, sekta za kilimo pia ukija bandani kwetu utapata huduma ya kupata TIN namba hapa hapa bandani,” amesema Kayombo.

Ameongeza kuwa, watakaotembelea pia wataelekezwa jinsi ya kutoa taarifa kwa wafanyakazi wasio na maadili ili waweze kuchukuliwa hatua.

“Wateja pia tutawaelewesha jinsi ya kuwaripoti wafanyakazi ambao hawana maadili na tunawaelimisha tunachukua hatua gani kwa watu hao ili waweze kufanya kazi kwa maadili,” amesema.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this