Lissu awaambia wafuasi wake wajiandae akitoka ni mchakamchaka

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amewaambia wasuasi na viongozi wa chama hicho  kuwa wajiandae  kwani  akitoka  ni mchakamchaka.

Lissu amezungumza hayo leo Julai 1, 2025 wakati alipokuwa anawasalimia   wafuasi na viongozi hao waliofika katika  Mahakama ya  Hakimu  Mkazi Kisutu kufuatilia  kesi ya uhaini  inayomkabili kiongozi huyo.

“Jiandaeni hii biashara tunaimaliza siku hizi hizi, nikitoka ni mchakamchaka, nikitoka tuko barabarani, hayo ya yule Jaji mwingine tutajuana nayo,” amesema Lissu  muda mchache baada ya kesi yake kuahirishwa, huku akiwatania wafuasi hao  kwa kusema  “Jamani mie mfungwa,”

Awali akiwa mahakamani hapo,  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franko Kiswaga, Lissu aliomba mahakama hiyo kuwa kama upelelezi ama ushahidi haujakamilika basi aachiwe huru kwa sababu mara ya mwisho waliambiwa upelelezi umekamilika na jalada lipo wa DPP.

Amesema  kuwa anaiomba mahakama hiyo isiahirishe kesi kwa sababu hakuna sababu ya msingi, kwani mara ya mwisho waliambiwa upelelezi umekamilika na wangepewa taarifa ya uamuzi.

Lissu alihoji kwamba inamchukua muda gani DPP kusoma faili la kesi hiyo hali ya kuwa yeye ni msomi wa sheria na kama upelelezi ama ushahidi haujakamilika basi aachiwe.

Akizungumzia  maisha yake ya Gerezani kwa sasa   mambo yamekaa vizuri, anapata  huduma za kiroho na pia anakutana na mawakili wake na anafanya mazoezi.

”Baada ya ku-demand hapa kesho yake Mkuu wa Gereza aliniita akaniambia utakaje, Jumapili inayofuata nilipata Padri kwenye selo yangu nikapata huduma ya kiroho.Bwana jela akasema kingine, nikamwambia nataka nifanye mazoezi mahali salama, akasema na hilo limepita kwa sasa nafanya mazoezi uwanjani napata hewa halisi.

“Na mawakili wangu kwa sasa tunakutana kwenye kachumba kamoja hivi, mambo yamekaa vizuri kabisa, lakini sisemi naenda vizuri  ili niendelee kukaa mule gerezani, hapana gerezani sio pazuri,” amesema Lissu.

Kwa upande wa Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga amesema kuwa kutokana na shauri hilo kuwa na maslahi kwa umma ndio maana wameomba ahirisho ili waje kusema kwamba jalada limefikia hatua gani.Pia DPP amefanya jitihada za kutosha kuhusu hiyo licha ya kuwa na majukumu mengi.

Kutokana na mvutano huo kwa kisheria, Hakimu Kiswaga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 15, 2025.

spot_img

Latest articles

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...

eGA yatumia Sabasaba kuelimisha umma kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho, yajivunia Tuzo ya Kimataifa

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) imeendelea kuonesha namna ambavyo Serikali inavyotekeleza mageuzi...

More like this

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...