Tanzania, Msumbiji  kuimarisha uhusiano kibiashara 

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia  Suluhu Hassan, amesema  Tanzania itaendelea kushirikiana na   Msumbiji katika  kuleta maendeleo , ustawi wa wananchi  ikiwamo kuimarisha  uhusiano kibiasharana  baina ya nchi hizo mbili na  kukuza mshikamano barani Afrika 

Akihutubia   katika  Sherehe za Madhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa  Msumbiji  leo Juni 25,2025 kwenye Uwanja wa Machava jijini Maputo, Rais Samia amesema  uhusiano wa  Tanzania na Msumbiji  si majirani tu bali ni ndugu  wa damu na uliimarishwa zaidi na Waasisi wa Mataifa hayo mawili.

Ameeleza kuwa  katika kuimarisha uhusiano  wa kibiashara, Shirika la Ndege  la Tanzania(ATCL), linatarajia  kuanzisha safari za  moja kwa moja  kati ya Tanzania na Msumbiji  mwaka huu.

“Katika kuzidi kufungua fursa zaidi za biashara baina ya wananachi wa Msumbiji na Tanzania, ninayo furaha kueleza kuwa, Shirika la Ndege la Tanzania linatarajia kuanza safari za ndege kati ya Tanzania na Msumbiji mwisho wa mwaka huu, hatua itakayoimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya watu wetu”, amesema Rais Samia.

Amesema  Bara la Afrika imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika hatua ya kwanza ya ukombozi, yaani uhuru wa kisiasa, hivyo kama viongozi wanapaswa kuhakikisha  nchi  zinakuwa na amani na umoja wa kitaifa ili  kuweza kushirikiana kufanikisha hatua nyingine za mageuzi ya kifikra, na kutafuta uhuru wa kiuchumi. 

Rais Samia amesema katika kufikia hatua hiyo ni njia mojawapo ni  kuhakikisha  watu wanaunganishwa pamoja na kuleta Umoja wa Kitaifa, hivyo anaamini chini ya uongozi wa Rais Daniel Chapo wa  Msumbiji wataendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo.

“Leo tunaposhuhudia ndugu zetu wa Msumbiji wakisherehekea Miaka 50 ya Uhuru wao, nasi ndugu zenu Watanzania tunashereheka pia. Ushindi wa Msumbiji ni ushindi wetu, mafanikio ya Msumbiji ni mafanikio yetu pia, na maendeleo ya Msumbiji ni maendeleo yetu sote,” ameeleza Rais Samia.

Aidha  amepongeza hatua ya maendeleo iliyofikiwa na Msumbiji katika  kipindi cha miaka 50, hasa nyanja za elimu afya na miundombinu ambayo yaliletwa na  dhamira ya kujenga jamii jumuishi na yenye matumaini.

Akizungumzia historia ya Uhuru wa nchi hiyo, Rais Samia amesema  Tanzania ilikuwa na mchango mkubwa  katika harakati za ukombozi wa  Msumbiji  kwa kuwapa hifadhi, licha ya  kukabiliwa na changamoto za  kiuchumi  na matishio kutoka kwa waliokuwa wakoloni.

“Tulikuwa  tayari kuchelewesha maendeleo  yetu ili kuhakikisha  ndoto ya  ukombozi Msumbiji na mataifa mengine ya Kusini mwa Afrika  inatimia,” amesema.

Katika hatua nyingine Rais Samia ametembelea  eneo la kumbukumbu ya Mashujaa wa Msumbiji, jijini Maputo  na kuweka  shada la maua kama ishara ya  heshima kwa Mashujaa waliopoteza maisha wakipigania Uhuru wa  nchi hiyo.

spot_img

Latest articles

Tumepata somo, tulitumie kukomesha wasiojulikana

LIPO tumaini. Ndivyo inavyoweza kuelezwa kwamba hata katika kiza cha usiku kuna tumaini la...

Yanga Bingwa Ligi Kuu msimu wa 2024/25

Na Mwandishi Wetu Yanga imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuichapa...

Malalamiko 461 Yawasilishwa EWURA Kwa Miaka Miwili

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema katika...

Wanaume wana haki ya kulindwa- IGP Wambura

Na Mwandishi Wetu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amesema wanaume nchini...

More like this

Tumepata somo, tulitumie kukomesha wasiojulikana

LIPO tumaini. Ndivyo inavyoweza kuelezwa kwamba hata katika kiza cha usiku kuna tumaini la...

Yanga Bingwa Ligi Kuu msimu wa 2024/25

Na Mwandishi Wetu Yanga imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuichapa...

Malalamiko 461 Yawasilishwa EWURA Kwa Miaka Miwili

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema katika...