Na Mwandishi Wetu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imemtangaza mwamuzi Amin Omar kutoka Misri kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo, Yanga dhidi ya Simba, utakaopigwa keshokutwa Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mwamuzi huyo ataisaidiwa na Mahmoud Ahmed, Samir Gamal Saad, mwamuzi wa akiba ni Ahmed Mahrous Elghandour wote kutoka Misri, wakati Kamishna wa mechi ni Salim Singano kutoka Tanga na mtathini waamuzi ni Alli Mohamed kutoka Somalia.
Mchezo huo utakaopigwa saa 11:00 jioni, ndio utaamua bingwa wa msimu 2024/25 ambapo kwa sasa Simba na Yanga zimepishana pointi moja.