Mke mkubwa ajiua na wanawe wanne kwa sumu kisa  mume  kumpendelea  huduma mke mdogo

Na Mwandishi Wetu

Mwanamke  aitwaye Kangw’a Tungu Mahigi(25) mkazi wa Kata ya Lugubu wilayani Igunga mkoani Tabora, amefariki yeye pamoja na watoto wake wanne kwa kunywa sumu aina ya Ruruka, inayotumika kuua wadudu,

huku  ikidaiwa chanzo cha vifo hivyo ikiwa ni mgogoro wa kifamilia.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, chanzo cha tukio hilo ni  ugomvi wa marehemu na mme wake  baada ya mume kudaiwa kuwa na upendeleo kwa mke mdogo ambaye amemjengea nyumba ya kisasa na kumpa huduma nyingine nzuri ambazo mke mkubwa na wanawe walikuwa hawazipati.

Amesema tukio hilo limetokea June 16, 2025  ambapo mwanamke huyo alimvizia mumewe akiwa shambani kisha kununua pakiti moja ya sumu hiyo na kunywa yeye na watoto wake.

Kamanda Abwao alitaja majina ya watoto waliofariki kuwa ni  Sengi James ( 8), Simon James ( 6), Elisha James ( 3) na Kashinje James (7).

Amesema kuwa mume wa marehemu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo, ikiwa ni pamoja na nafasi yake katika muktadha wa mgogoro wa kifamilia uliokuwepo kabla ya tukio.

Kamanda huyo ameeleza kuwa nyumbani kwa marehemu ilikutwa pakiti moja ya sumu hiyo ambayo imetumika pamoja na kikombe cha plastiki chenye sumu, ambapo miili ya marehemu ili hifadhiwa mochwari Igunga kwa ajili ya uchunguzi na baadae kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

“Hili ni tendo la kikatili,  kihalifu na lisilo na utu lililoangamiza  maisha ya watu wasiostahili kuumizwa na pia linaondoa nafasi ya mtu mwenye matatizo kupata msaada wa  kweli. Jeshi la Polisi mkoani Tabora linalaani na kuendelea kutoa wito kwa jamii, pale inapojitokeza migogoro mbalimbali kutumia viongozi wa dini, Serikali na dawati la jinsia kutafuta ufumbuzi.” amesema.

spot_img

Latest articles

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...

eGA yatumia Sabasaba kuelimisha umma kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho, yajivunia Tuzo ya Kimataifa

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) imeendelea kuonesha namna ambavyo Serikali inavyotekeleza mageuzi...

More like this

Waziri Aweso: Tuna uhakika wa maji ya kutosha Dar na Pwani

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewatoa hofu wakazi wa mikoa ya...

PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia...

Machungu, damu yamwagwa tena

Maadhimisho ya Saba Saba nchini Kenya ni tukio muhimu katika kukumbuka mapambano ya kudai...