DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza kilogramu 504.36 za dawa za kulevya aina ya heroin katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara.

Uteketezaji huo umefanyika kufuatia amri ya Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Mtwara baada ya kukamilika kwa hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa waliohusika na dawa hizo.

Dawa hizo zilikamatwa ndani ya jahazi la Al Arab lililokuwa na raia saba wa Iran katika Bahari ya Hindi ndani ya eneo la kiuchumi la Tanzania.

Uteketezaji huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Sura ya 95 inayoruhusu kuteketezwa kwa vielelezo vya dawa za kulevya baada ya taratibu za kisheria kukamilika au wakati shauri linaendelea kwa idhini ya mahakama.

Sambamba na hatua hiyo, Mamlaka imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha huduma za tiba na utengemao kwa watu wenye uraibu wa dawa za kulevya hususan katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.

Katika kutekeleza azma hiyo, DCEA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuwezesha upatikanaji wa huduma za MAT pamoja na kuanzishwa kwa nyumba za upataji nafuu (sober houses) ili kusaidia waraibu kupata huduma stahiki na kurejea katika maisha yenye tija kwa jamii.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya itaendelea kushirikiana na vyombo vya dola, wadau mbalimbali pamoja na wananchi katika kuzuia usafirishaji, biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Aidha, Mamlaka itaendelea kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma kuhusu madhara ya dawa za kulevya na umuhimu wa ushiriki wa jamii katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

spot_img

Latest articles

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

COASCO: Ukaguzi wa vyama vya ushirika waongeza uwazi na kuimarisha imani ya wanachama

Na Tatu Mohamed Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limesema ukaguzi...

More like this