DAWASA yasisitiza matumizi ya bidhaa za ndani kuimarisha huduma ya maji

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema itaendelea kuunga mkono matumizi ya bidhaa zinazozalishwa na wazalishaji wa ndani, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza uchumi wa taifa sambamba na kuimarisha upatikanaji wa vifaa vinavyosaidia utoaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire, alipofanya ziara katika kiwanda cha Lake Steel Company Ltd kilichopo Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, kwa lengo la kujionea uzalishaji wa malighafi na mabomba yanayotumika katika miradi ya maji.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mhandisi Bwire amesema DAWASA inaamini katika kuviunga mkono viwanda vya ndani vinavyozalisha vifaa muhimu kwa sekta ya maji, hatua ambayo si tu inasaidia kuboresha huduma kwa wananchi bali pia kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Leo tumekuja kuwatembelea wazalishaji wa malighafi muhimu katika sekta ya maji ambao huzalisha mabomba yanayotumika kusambaza huduma kwa wananchi. Tumejionea teknolojia za kisasa wanazotumia pamoja na ubora wa bidhaa zao, hivyo tunaamini katika kuwaunga mkono wazalishaji wa ndani ili kukuza viwanda vya ndani na uchumi wa taifa,” amesema Mhandisi Bwire.

Aidha, amesema matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini yataongeza upatikanaji wa vifaa kwa haraka, kupunguza gharama za uagizaji kutoka nje ya nchi na kusaidia utekelezaji wa miradi ya maji kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Lake Steel Company Ltd, ndugu Awdhesh Kumar, ameishukuru Serikali kupitia DAWASA kwa kutembelea kiwanda hicho na kujionea uwezo wa uzalishaji pamoja na teknolojia zinazotumika katika utengenezaji wa mabomba ya maji.

“Kampuni yetu imejikita katika kuzalisha bidhaa zenye ubora wa viwango vya kitaifa na kimataifa ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya maji kwa ufanisi mkubwa. Tunaamini ushirikiano kati ya DAWASA na Lake Steel utaongeza kasi ya maendeleo ya sekta ya maji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi,” amesema Kumar.

Ziara hiyo inaakisi dhamira ya DAWASA ya kuendelea kushirikiana na sekta binafsi pamoja na wazalishaji wa ndani katika kuhakikisha huduma ya majisafi inawafikia wananchi kwa ufanisi na kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini.

spot_img

Latest articles

Ofisi ya Msajili wa Hazina yatoa wito wa utawala bora kuimarisha uwekezaji wa umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) imesisitiza kuwa mustakabali wa mafanikio...

TTB yamkaribisha bingwa wa Masumbwi duniani Terence kwa ziara ya utalii

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amemkaribisha nchini...

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

More like this

Ofisi ya Msajili wa Hazina yatoa wito wa utawala bora kuimarisha uwekezaji wa umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) imesisitiza kuwa mustakabali wa mafanikio...

TTB yamkaribisha bingwa wa Masumbwi duniani Terence kwa ziara ya utalii

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amemkaribisha nchini...

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...