Rais Samia: Mwelekeo ni elimu ya ujuzi kwa vijana kumudu soko la ajira

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya CCM anayoiongoza, imechukua hatua madhubuti katika kuweka mwelekeo wa elimu itakayotoa ujuzi na stadi za kazi kwa vijana ili kuwapatia sifa katika soko la ajira.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, Juni 18, 2025, wakati alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Amali ya Sekondari Mwamapalala, Wilaya ya Itilima, kwa niaba ya shule zote 103 za sekondari za amali zinazojengwa maeneo mbalimbali, nchini.

“Shule hizi na elimu ya ufundi stadi tunalenga zitoe elimu ya ujuzi kwa vijana wetu ili wanapomaliza wawe na sifa katika soko la ajira, kuajiriwa au kujiajiri. Shule hii tutaanza masomo ifikapo mwezi Januari mwakani,” amesema Rais Samia.

Pia amewapongeza wananchi wa Itilima jinsi wilaya yao inavyopiga hatua za maendeleo kwenye sekta mbalimbali, huku akiwasisitiza umuhimu wa kuwapatia watoto wao fursa za kupata elimu, wakitumia ipasavyo miundombinu inayojengwa kwa gharama kubwa na Serikali yao.

“Ndugu wananchi wenzagu wa Itilima kwanza nawapongeza sana kwa hatua kubwa za maendeleo mliyonayo. Leo nimeweka jiwe la msingi kwa niaba ya shule zingine zote za amali zinazojengwa nchini. Nitakapozindua zikikamilika kujengwa, pia nitazindua kwa niaba ya shule zote nchini.

Rais Samia anaendelea na ziara yake yake ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu, leo ikiwa ni siku ya nne tangu alipoanza siku ya Jumapili, Juni 15, 2025.

spot_img

Latest articles

Dk. Mwigulu ajadiliana na Kamati ya Maandalizi AFCON 2027

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi...

Coastal Union yawatembezea kichapo maafande wa Magereza

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Coastal Union imetembeza kichapo cha mabao 4-1 kwa maafande wa...

Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna...

Msajili wa Hazina aikaribisha Jeune Afrique Media Group kuangazia fursa za uwekezaji

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Frederic...

More like this