Mwanafunzi wa chuo ashikiliwa Polisi kwa kumuua mwenzake  wakiwa ‘Club’ wamelewa

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must), mwaka wa kwanza, Emilia Joseph (21) kwa tuhuma za mauaji ya mwenzake wakiwa kwenye ‘Club’ ya Mbeya Pazuri jijini humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amedai kuwa mtuhumiwa alifanya mauaji ya mwenzake wa mwaka wa tatu Gerald Philber Said (22), baada ya kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne Juni 17,2025,  imesema tukio hilo lilitokea Juni 14,2025 saa 11.00 alfajiri wakiwa wamelewa pombe kupita kiasi.

Amedai kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni baada ya kuibuka ugomvi baina ya marehemu na mtuhumiwa uliotokana na matumizi ya ulevi wa pombe kupindukia.

” Baada ya kuibuka ugomvi mabaunsa walimtoa mtuhumiwa nje ambaye alienda kwenye eneo alikoegesha gari , ambapo marehemu alimfuata kwa lengo la kuendeleza ugomvi ndipo alipomchoma na kitu chenye ncha kali tumboni ,”amesema.

Amesema baada ya marehemu kubainika kudhurika ndipo wasamaria wema walimbeba na kumuwahisha katika Hospitali ya Rufaa Kanda kwa matibabu zaidi.

“Wakati madaktari wakiendelea kumpatia matibabu ilipofika saa 7.00 mchana alifariki dunia,”amesema.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Kuzaga ameonya wanafunzi wa vyuo vikuu kuachana na matumizi ya pombe kupitia kiasi na badala yake kuzingatia masomo na kutimiza ndoto zao.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

More like this