Kocha Yanga: Siwaandai wachezaji wangu kisaikolojia kwa sababu si wagonjwa, tuna fainali nne za kucheza  

Na Mwandishi Wetu

Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamad amesema hawaandai wachezaji wake kisaikolojia kwa sababu si wagonjwa,  wako vizuri kiakili, yeye kama kocha kazi yake ni kuwaandaa kimbinu na kuwa fiti

Miloud ametoa  kauli hiyo, leo Juni 17, 2025 kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara  dhidi ya Tanzania Prisons unatarajiwa kupigwa kesho, kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Kocha huyo ametamba kuwa  wana fainali nne za kucheza  na mojawapo ni mchezo huo na Prisons, wamejiandaa vizuri kukabiliana na wapinzani  wao kuhakikisha wanapata ushindi.

“Maandalizi yetu yapo vizuri sana, tuna fainali nne za kucheza. Tupo tayari kuukabili mchezo wa kesho kikamilifu. Kila mchezaji anajua kitu gani cha kufanya kesho, kikosi chetu kipo kamili hakuna majeruhi wapya. Hatuna presha yoyote na hatuna sababu ya kuwa na presha.

“Tunaheshimu sana Tanzania Prisons, lakini sisi ni Yanga. Nina wachezaji wenye uzoefu na uwezo mkubwa. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini hatuna sababu ya kuwaza sana kuhusu hilo. Tumekuja kushindana kwa tahadhari kubwa,” amesema kocha huyo.

Aidha amewashukuru mashabiki  wa timu hiyo  kwa sapoti yao kubwa kwa kuwa amefanya kazi na klabu nyingi lakini wa Yanga wamekuwa tofauti kutokana na kujitoa kila sehemu timu inapokwenda.

“Tumekuja Mbeya kusaka alama tatu tunawashukuru sana mashabiki, nimefanya kazi Klabu mbalimbali kubwa lakini mashabiki wa Yanga ni mashabiki wa mfano. Naamini kesho kwa mchango wao Uwanjani basi tutakuwa na wakati mzuri. Niwaombe sana mashabiki wajitokeze kwa wingi,” 

Kwa  upande wake  kocha wa  Tanzania Prisons, Amani Josiah amesema   wamejiandaa kucheza na timu ambayo iko imara, lengo lao ni kutumia faida ya kucheza nyumbani kuepuka  kucheza mechi za mtoano ‘play off’

Amesema  kutakuwa na mabadiliko kimbinu  kulingana na aina ya timu wanayokutana nayo, pia hawana majeruhi katika kikosi chao ambapo wachezaji waliokosekana kwa muda mrefu tayari  wamerejea.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...