Rais Mwinyi: SMZ imeweka mkazo kuifungua Pemba kiuchumi

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali imeweka mkazo maalum wa kuifungua Pemba kiuchumi kupitia ujenzi wa uwanja wa ndege, bandari na miundombinu ya barabara.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Ujumbe Maalum wa Serikali ya Uingereza, ukiongozwa na Kate Osamor (MB), Mjumbe Maalum wa Biashara wa Serikali ya Uingereza kwa Afrika Mashariki.

Katika mazungumzo hayo Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa ujenzi wa miundombinu ya barabara umefikia asilimia 70, sambamba na maendeleo ya ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Pemba pamoja na bandari.

Akizungumzia kilimo cha mwani ambacho kina mwamko mkubwa kwa wanawake wa Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa licha ya ongezeko la uzalishaji wa zao hilo, bado bei ya mwani hairidhishi kulingana na juhudi zinazowekwa na wazalishaji.

Ameutaka ujumbe huo kuangalia njia bora ya kuwawezesha wazalishaji kwa kuongeza thamani ya zao hilo.

Rais Dkt. Mwinyi ametoa rai kwa ujumbe huo kwamba Zanzibar bado inahitaji wawekezaji zaidi kutoka sekta binafsi ili kufikia Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050.

Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Balozi Marianne Young, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kasi ya maendeleo yanayofikiwa Zanzibar katika sekta mbalimbali za uchumi, na kuahidi kuendeleza ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this