Mambo bado magumu dabi ya Kariakoo, Yanga yaikomalia Bodi ya Ligi

Na Mwandishi Wetu

Licha ya kufanya kikao na uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), leo Juni 9, 2025, Klabu ya Yanga imeendelea  kushikilia msimamo wake kuwa haitacheza  mechi  ya Juni 15,2025 dhidi ya Simba endapo  hawatakapotimiziwa matakwa yao.

Kikao hicho kimefanyika ikiwa zimebaki  siku sita pekee kufikia tarehe ya mchezo huo ambao awali ulitakiwa kuchezwa Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa  iliyotolewa na Kamati ya Utendaji ya Yanga leo, imesema kuwa msimamo wao hautobadilika hadi pale mahitaji yao yatakapotimizwa.

Akizungumzia yaliyojili katika kikao hicho, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,  Almas Kasongo, amesema kuwa kikao cha leo kilikuwa  kwa ajili ya   kupokea matakwa ya Yanga ambayo ni  manne,  kujiuzulu kwa Mwenyeketi wa bodi ya ligi, kujiuzulu kwa Ofisa mtendaji mkuu wa, Katibu mkuu wa Tff na kuona bodi ya ligi kuu inakuwa chombo huru.

“Hivyo basi matakwa hayo yamepokewa na yatawasilishwa kwa shirikisho la soka nchini  TFF, ila kwa mamlaka ya bodi ya ligi mpaka sasa ni mchezo upo pale pale juni 15,” amesema.

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this