Dkt. Biteko aitaka jamii ijipange kuepusha migogoro

📌 Azindua kitabu cha miaka 35 ya TAWLA

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka wanajamii kujiepusha na mazingira yanayoweza kusababisha migogoro baada ya wao kufariki.

Biteko amesema hayo leo Mei 23, 2025 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).

Amesema endapo wanajamii watajiandaa na kuweka mazingira mazuri, wataepusha migogoro isiyo ya lazima na jamii itaishi kwa amani na kupunguza gharama zinazotumika kurekebisha jamii yenye migogoro.

Aidha, ameipongeza TAWLA kwa kazi nzuri iliyodumu kwa miaka 35 tangu kuazishwa kwake mwaka 1990.

“Tangu mlipoanzishwa kuna vyama vingi vya kijamii vilianzishwa sambamba na chama chenu, lakini vingine vilikufa baada ya mwaka mmoja, vingine vilikufa baada ya miaka mitano na vingine vilisambaratika baada ya miaka 10. Ninyi mmeimarika na kukua hadi leo na mnaendelea kufanya kazi nzuri,” ameongeza Dkt. Biteko.

Pia amewasilisha pongezi za Rais Samia kwa TAWLA kupitia kushiriki kampeni ya msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na upendo kama ilivyo ndoto ya TAWLA ya kuwasaidia watu wenye uhitaji.

“Bila mchango wenu, mafanikio yanayozungumzwa serikalini huenda yasingekuwa yanazungumzwa kwa kiwango hicho, amesema Dkt. Biteko.

Ameutaka uongozi wa TAWLA kuendelea kuwashawishi na kuwavutia wanachama wapya watakaoweza kutoa msaada bila kusita katika jamii yao.

Amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha wanawake wanakuwa katika nafasi mbalimbali za maamuzi ikiwemo kuongeza uwiano wa majaji wanawake na wanaume katika Mahakama za Rufani na Mahakama Kuu.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu ujao, Dkt. Biteko amewahimiza wajumbe wenye nia kujitokeza na kugombea uongozi ili kuwakilisha wananchi hususan wanawake wanaongezeka.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza TAWLA kwa kazi ya kutetea kundi maalum la wanawake na kuliwezesha kupata msaada wa kisheria.

“TAWLA inafanya kazi kubwa ya kufanyia kazi tabia za watu na kazi hiyo inahitaji mawanda mapana” amesema na kuongeza kuwa wadau wa sheria wanashughulia watu wenye malezi na makuzi tofauti hivyo, kazi yao ni kubwa inayohitaji kufanyika kwa weledi wa hali ya juu.

Mwenyekiti wa TAWLA, Wakili Suzan Ndomba ameipongeza Serikali kwa hatua zake za kulinda haki na kushughulikia changamoto za zinazowakabili wanawake na watoto nchini.

Amesema hatua ya Serikali kuwekeza katika utekelezaji wa miradi ya nishati, maji na elimu ni fursa zaidi kwa kundi la wanawake wa Tanzania ambao wamekuwa waathirika wakubwa madhara yanayotokana na ukosefu wa miundombinu hiyo.

Amefafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa TAWLA, chama hicho kimeshiriki kutoa mafunzo kwa baadhi ya mawakili, kuanzisha huduma ya simu ya bure kwa ajili ya wateja wake kurupoti vitendo na matukio ya ukatili, kuwatetea wateja wake mahakamani, kushiriki katika kuandaliwa na kutungwa kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009 pamoja na kutungwa kwa kifungu maalum cha makosa ya kujamiiana SOSPA (2008).

spot_img

Latest articles

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango afanya mazungumzo na Rais wa AfDB anayemaliza muda wake

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amekutana na...

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango afanya mazungumzo na viongozi mbalimbali Ivory Coast

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akizungumza na...

More like this

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango afanya mazungumzo na Rais wa AfDB anayemaliza muda wake

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amekutana na...

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango afanya mazungumzo na viongozi mbalimbali Ivory Coast

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akizungumza na...