Na Mwandishi Wetu
Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, ametangazwa ni Kardinali Robert Francis Prevost(69), raia wa Marekani na amechagua jina la Papa Leo XIV.
Amechaguliwa leo Mei 8,2025, kuchukua nafasi ya Papa Francis,aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, Aprili 21, 2025.
Moshi mweupe ulionekana jioni ya leo katika bomba lililopo katika paa la kanisa la Sistine Chapel mjini Vatican, ukiashiria kuwa tayari Makardinali walioketi kuanzia jana Mei 7,2025, wamempata Papa mpya.