Na Mwandishi Wetu
Timu ya Simba imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya leo kutoka suluhu na Stellebosch katika mchezo wa nusu fainali ya pili uliopigwa nchini Afrika Kusini.
Simba imeingia fainali kwa wastani wa bao 1-0 kutokana na ushindi katika mchezo wa kwanza uliopigwa dimba la Mkapa, Dar es Salaam.