Kiungo fundi Yanga kuikosa Azam

Na Mwandishi Wetu

Kiungo wa Yanga Khalid Aucho atakosekana katika mchezo  wa Ligi Kuu Bara  dhidi ya Azam kutokana na jeraha la nyama ya paja alilopata wakati wa mechi dhidi ya Coastal Union ambapo alishindwa kuendelea na mchezo.

Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe amethibitisa kukosa huduma ya nyota huyo baada ya kufanyiwa vipimo mbalimbali leo na kubainika kuwa na shida ya nyama za paja ambapo  ambapo atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu.

“Siku ya leo tukiongozwa na daktari wetu, Moses Itutu, tulikwenda kwenye hospitali ya  Saifee na Khalid Aucho akafanyiwa vipimo tofauti tofauti na kugundulika amepata shida ya nyama za paja sehemu ya nyuma. Lakini taarifa ya daktali ni kwamba hatakuwepo kwenye mchezo wetu na Azam,”  amesema Kamwe.

Yanga inatarajia kukutana na Azam Aprili 10, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

More like this

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...