Na Mwandishi Wetu
Kiungo wa Yanga Khalid Aucho atakosekana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam kutokana na jeraha la nyama ya paja alilopata wakati wa mechi dhidi ya Coastal Union ambapo alishindwa kuendelea na mchezo.
Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe amethibitisa kukosa huduma ya nyota huyo baada ya kufanyiwa vipimo mbalimbali leo na kubainika kuwa na shida ya nyama za paja ambapo ambapo atakaa nje ya uwanja kwa wiki tatu.

“Siku ya leo tukiongozwa na daktari wetu, Moses Itutu, tulikwenda kwenye hospitali ya Saifee na Khalid Aucho akafanyiwa vipimo tofauti tofauti na kugundulika amepata shida ya nyama za paja sehemu ya nyuma. Lakini taarifa ya daktali ni kwamba hatakuwepo kwenye mchezo wetu na Azam,” amesema Kamwe.
Yanga inatarajia kukutana na Azam Aprili 10, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.