SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI-MAJALIWA

Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kufanya maboresho zaidi ya mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuifanya Tanzania iendelee kuwa sehemu salama zaidi ya uwekezaji.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Aprili 3, 2025, wakati wa uzinduzi wa Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini (MKUMBI II) katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Amesema kupitia mpango ambao ameuzindua, maandalizi yake pamoja na kamati zake, Serikali itaweza kushughulikia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii, na kiteknolojia na kuweka mazingira bora zaidi kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

“Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa wadau wote ili kufanikisha malengo ya kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara. Ni mategemeo yetu kuwa, mpango huu utaongeza tija kubwa kwa Taifa letu na kusaidia kufikia malengo yetu ya kuwa na uchumi wa kati ulio endelevu.”

Akizungumza kuhusu umuhimu wa MKUMBI II, Waziri Mkuu amesema kuwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji wa nje na ndani, kuongeza fursa za ajira, kuboresha miundombinu, upatikanaji wa soko la kimataifa kwa bidhaa za ndani, kukuza ushindani na ubora wa bidhaa.

Aidha, Majaliwa ametumia fursa hiyo kuisisitiza kamati ya maandalizi ya MKUMBI II iharakishe maandalizi ya mpango huo ili utekelezaji wake uweze kuanza mara moja na kurahisisha mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji.

Pia, Waziri Mkuu amezitaka Taasisi na Mamlaka za Udhibiti za Serikali ambazo zitahusishwa katika utafiti na tathmini zitoe ushirikiano wa dhati kwa kamati ili iweze kuja na mapendekezo mahsusi yenye malengo mapana ya nchi ambayo yataendana na Dira ya Taifa 2050.

Kwa upande wake, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema lengo la Serikali la kuandaa mpango huo ni pamoja na kuona kuwa Tanzania inakuwa sehemu bora na ya kuvutia ya kufanya biashara na uwekezaji. “Kazi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ni kazi endelevu.”

spot_img

Latest articles

ALLY KAMWE  AKAMATWA NA POLISI AACHIWA  KWA DHAMANA

Na Mwandishi Wetu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao amesema Jeshi la...

Bado watu wanapotea, yu wapi wa kuzuia hali hii?

ASKOFU wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dk. Benson...

Dkt. Biteko ashiriki uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Pwani

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo Aprili 2, 2025...

More like this

ALLY KAMWE  AKAMATWA NA POLISI AACHIWA  KWA DHAMANA

Na Mwandishi Wetu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao amesema Jeshi la...

Bado watu wanapotea, yu wapi wa kuzuia hali hii?

ASKOFU wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dk. Benson...