Serikali: Faida itokanayo na uwekezaji ifikie zaidi ya asilimia 10

Na Mwandishi Wetu, Pwani

SERIKALI inataka faida itokanayo na uwekezaji ‘return on investment’ katika kampuni ambazo serikali inaumiliki wa hisa chache kuongezeka kutoka asilimia saba ya sasa hadi kufikia zaidi ya 10 mwaka ujao wa fedha.

Dhamira hiyo ilielezwa Ijumaa, Machi 28, 2025, na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka wilayani Kibaha, mkoani Pwani, wakati wa kufunga mkutano wa siku tatu wa wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo serikali inaumiliki wa hisa chache.

“Niwape changamoto ya kukuza rudisho la uwekezaji kutoka asilimia saba ya sasa kwenda zaidi ya asilimia 10 kwa mwaka. Na ili kufikia azma hii mnapaswa kuongeza ufanisi wa utendaji,” alisema.

Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia jumla ya taasisi 308 ambapo kati ya hizo 56 ni zile ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache.

Jumla ya uwekezaji wa Sh86.3 trilioni umefanywa katika taasisi hizo, huku kati ya kiasi hicho Sh2.9 trilioni zikiwekezwa kwenye kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache na Sh83.4 trilioni kikienda kwa taasisi ambazo serikali ina umiliki wa asilimia 100.

Aidha, Balozi Kusiluka aliwapa changamoto wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina hisa chache kuongeza ufanisi gawio kwa serikali.

“Ninaamini mwaka ujao wa fedha nitaona gawio kutoka Taasisi mnazosimamia likiongezeka. Hiyo ni changamoto ninayowaachia,” alisema wakati wa mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Kwa mwaka wa fedha uliopita, serikali ilipata gawio la Sh195 bilioni kutoka kampuni zake ambazo ina umiliki wa hisa chache, kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina.

“Mafanikio yetu yataakisi juhudi za Serikali chini ya Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambazo zimekuwa zikifanyika za kuweka mazingira rafiki na wezeshi ya biashara,” alisema Dk Kusiluka.

Alionesha imani yake kwa mwongozo ulioboreshwa wa Wakurugenzi wa Bodi wa Hisa chache uliozinduliwa Jumatano wiki hii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere.

“Nimeupitia kwa kina na nimeona umejaa mingozo mizuri itakayotusaidia kutekeleza majukumu yetu kwa weledi na kwa wakati,” alisema Dk. Kusiluka, huku akiipongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kutengeneza Mwongozo huo.

Ni katika muktadha huo aliwaelekeza wakurugenzi wa bodi kuutumia kikamilifu ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amewataka wawakilishi wa serikali kwenye bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa hisa chache kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Aliwataka wawakilishi hao ambao ni wakurugenzi wa bodi kuzitendee haki nafasi walizopewa ili kuhakikisha kuwa serikali inanufaika na uwekezaji iliofanya kwenye kampuni ambazo ina umiliki wa hisa chache.

“Nyie ni jicho la serikali hivyo mnapaswa kutokuchukulia kiwepesi nafasi mlizopewa, vinginevyo mtakuwa hamuitendei haki serikali na watanzania wote kwa ujumla,” Mchechu aliwaambia wakurugenzi hao.

Aliongeza: “Lazima mjidhatiti na kama unaona hauko kwenye nafasi ya kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na muda wa kutosha, ni vyema ukasema ili nafasi hiyo wapewe wengine,”.

spot_img

Latest articles

ELIMU YA VIPIMO YAWAVUTIA WANANCHI, WAAHIDI KUWA MABALOZI WA KUJITOLEA

Na Mwandishi Wetu Dodoma – “Sasa najua ni nini ninapaswa kuangalia ninapojaza mafuta, kununua...

Bodi ya DAWASA yasisitiza kukamilika kwa wakati ufungaji pampu mpya za maji

Na Mwandishi Wetu BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira...

JAB YASOGEZA HUDUMA ZA ITHIBATI KARIBU NA WAANDISHI DODOMA

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeanza kutoa huduma...

Wadau wavutiwa elimu ya vipimo maadhimisho wiki ya utumishi wa umma

Na Mwandishi Wetu WADAU mbalimbali waliotembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika siku ya...

More like this

ELIMU YA VIPIMO YAWAVUTIA WANANCHI, WAAHIDI KUWA MABALOZI WA KUJITOLEA

Na Mwandishi Wetu Dodoma – “Sasa najua ni nini ninapaswa kuangalia ninapojaza mafuta, kununua...

Bodi ya DAWASA yasisitiza kukamilika kwa wakati ufungaji pampu mpya za maji

Na Mwandishi Wetu BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira...

JAB YASOGEZA HUDUMA ZA ITHIBATI KARIBU NA WAANDISHI DODOMA

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeanza kutoa huduma...