Waziri Kitila ataka mabadliko sheria ya uagizaji magari kulinda viwanda vya ndani

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuna haja ya kurekebisha Sera katika sheria za uagizaji wa magari ili kulinda viwanda vya  utendenezaji magari nchini.
 
Prof. Kitila ameyasema hayo wakati leo Machi 27,2025 alipotembelea kiwanda cha kutengeneza  magari nchini  cha GF Vehicle Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Akiwa ameambatana na viongozi wa TCI, Waziri Mkumbo ametembelea kiwanda hicho na kujionea namna kinavyounganisha magari hayo kuanzia hatua ya mwazo hadi linakamilika na alifanikiwa kushuhudia uzinduzi wa gari ya 3400 ikiwa ni toka kuanzishwa kwa kiwanda hicho.
 
Akizungumza wakati wa ziara hiyo  Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho , Ezra Mereng amewasilisha hoja ya maombi kwa serikali ya kubadilishwa kwa sera na sheria za uagizaji wa magari nchini ili kulinda viwanda vya ndani.

 Amesema wao kama kampuni wanafanya upanuzi wa kuingia awamu ya 3 ambayo inategemewa kufanya uwekezaji wa mtaji wa zaidi ya sh 10 bilioni na hadi sasa imeajiri zaidi ya vijana 200 na katika awamu ya 3 wanatarajia kuajiri zaidi ya vijana 300 wa ajira ya moja kwa moja.
 
Katika awamu hii tunahitaji vitu vingi vipatikane nchini kama chuma na vifaa vingine kwa mfano, tumeshaanza kununua betri za magari kutoka katika kiwanda kimoja wapo nchini  sasa bila kufanyika kwa mabadiliko ya sheria za kulinda viwanda vya ndani ni kazi bure.
 
“Kwa sasa kumekuwa na uagizaji holela wa magari na katika hili Tanzania tunakuwa walaji wa mwisho kwa kuwa magari mengi ni ya mtumba (used), pia kukiwa na sheria ya manunuzi na usimamizi kwa miradi mikubwa ya nchi basi lazima magari au vifaa vitakavyotumika vinunuliwe nchini hii itasaidia kuvilinda viwanda vyetu,” ameeleza Ezra.
 

spot_img

Latest articles

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

More like this

Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

Na Winfrida Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O...

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...