MCHENGERWA ATOA MIEZI MIWILI BARABARA ZA TARURA IKWIRIRI ZIKAMILIKE

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold Runji, kuhakikisha wakandarasi wanakamilisha ujenzi wa barabara za lami Ikwiriri ndani ya miezi miwili ili wananchi wanufaike na maboresho ya miundombinu hiyo.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo wilayani Rufiji.

“Natoa miezi miwili tu, barabara ziwe zimekamilika ifikapo Mei 30, 2025, ikiwa ni pamoja na mitaro na taa za barabarani. Hakutakuwa na nyongeza ya muda,” amesisitiza.

Ameagiza Meneja wa TARURA kuwasimamia wakandarasi wafanye kazi usiku na mchana, akibainisha kuwa barabara hizo zilipaswa kukamilika Desemba 2024 na iwapo hazitakamilika kwa muda uliopangwa, atamuwajibisha meneja huyo.

Nao, Baadhi ya wananchi, akiwamo Dereva wa bodaboda Ramadhan Mwipi na Mama Lishe Mariam Hamza, wamemshukuru Waziri Mchengerwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha barabara hiyo, wakieleza kuwa imeleta ahueni kubwa kwa usafiri na biashara zao.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya...

More like this