Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali ya uchumi wa Tanzania imeendelea kuimarika na kuwa himilivu.

Gavana Tutuba ameyasema hayo Machi, 20 2025 jijini Dar es Salaam katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa wananchi na wadau mbalimbali.

Imefanyika makao makuu ya BoT jijini Dodoma, makao makuu ndogo Zanzibar, matawi ya Mtwara, Mwanza, Arusha na Mbeya.

“Mpaka sasa, Tanzania imeendelea kung’ara katika medali za kiuchumi kidunia. Hali yetu ya uchumi, imeendelea kuwa nzuri katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Fedha ambayo imeendelea kuimarika, imeendelea kuwa na utulivu, imeendelea kuwa thabiti.

“Imeendelea kuwa na mtaji mkubwa na ukwasi wa kutosha na pia ina ufanisi mzuri wa viwango vya kimataifa na inajiendesha kwa faida,” amesema Gavana Tutuba.

Amesema, kwa kipindi cha miaka mitatu Sekta ya Uchumi na Fedha nchini imeendelea kufanya vizuri.

“Na kwa takwimu tunafahamu kwamba, kwa mwaka 2024 uchumi wa nchi yetu ulikuwa kwa takribani asilimia 5.4 ikilinganishwa na ukuwaji wa uchumi wa kidunia ambao ulikuwa asilimia 3.2.Kwa hiyo tumefanya vizuri,” amesema.

Aidha, kwa upande wa mfumuko wa bei, Gavana Tutuba amesema ulikuwa asilimia 3.1 ukilinganishwa na mfumuko wa bei wa kidunia wa asilimia 4.7.

Kwa upande wa ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, Gavana Tutuba amesema, mambo yalikuwa mazuri, kwani likuwa kwa asilimia 16.8 ikilinganishwa na lengo la asilimia 15.

Kutokana na changamoto hiyo, Gavana Tutuba ametoa wito kwa wananchi wote kujiepusha na shughuli za upatu.

Pia, amewataka wananchi kuhakikisha wanapata huduma za mikopo kwa watoa huduma wenye leseni halali kutoka Benki Kuu au kupitia taasisi zilizokasimishwa mamlaka.

“Kwenye halmashauri kwa leseni za VICOBA na kwenye Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa leseni za SACCOS,” amesema.

Pia, amewataka watoa huduma za mikopo wenye leseni kuhakikisha wanatoa huduma sahihi na ambazo haziwaumizi wananchi.

Amesema, kwa yule ambaye atakwenda kinyume na leseni yake, Benki Kuu itachukua hatua ikiwemo kumfutia leseni husika.

Kuhusu mfungo, Gavana Tutuba amesema, kwa upande wa kiroho, viongozi wengi wa kidini zote za Kiislamu na Kikristo wameendelea kufundisha hiki ni kipindi muhimu ambacho mwanadamu anapaswa kumrejea Mungu wake.

“Kipindi hiki cha mfungo ninafahamu ni kipindi muhimu sana katika maisha ya mwanadamu na kipindi ambacho kina faida nyingi za kiroho na kimwili. Ni kipindi ambacho kinatupatia fursa na Mwenyezi Mungu kwa sala, maombi na hata kutafakari ukuu wa Mwenyezi Mungu,” amesema.

Naye Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zuber, ameitaka Benki Kuu kuendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi katika matumizi ya huduma za fedha.

Amesema, kupitia elimu ya fedha kwa wananchi itawapa uwanda mpana wa kuweza kutambua sehemu sahihi za kupata mikopo.

Pia, amesema elimu hiyo itasaidia wananchi kuendesha biashara zao kwa faida.

“Kwa hiyo msiache kutoa elimu hii, ili iweze kufikia mahali ambapo mwananchi anaweza kufanya shughuli zake kwa utulivu,” amesema.

Amewahimiza wananchi kuendelea kudumisha amani nchini hasa kipindi hiki Taifa linaelekea katika Uchaguzi Mkuu.

spot_img

Latest articles

Dkt Biteko: Serikali kuendelea kuwekeza katika sekta ya Afya

📌 Dkt. Biteko atambelea Hospitali ya Wilaya ya Meru Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeahidi kuendelea...

THRDC yashauri kuitishwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)...

Sh. Bilioni 30 zaidhinishwa kujenga Barabara zilizoathiriwa na mvua

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kutumia kiasi cha...

Ewura yazitaka kampuni za gesi kuongeza mawakala, kudhibiti uchakachuaji wa gesi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za nishati na...

More like this

Dkt Biteko: Serikali kuendelea kuwekeza katika sekta ya Afya

📌 Dkt. Biteko atambelea Hospitali ya Wilaya ya Meru Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeahidi kuendelea...

THRDC yashauri kuitishwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)...

Sh. Bilioni 30 zaidhinishwa kujenga Barabara zilizoathiriwa na mvua

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kutumia kiasi cha...