Kapinga: Maeneo ya kijamii yamepewa kipaumbele kufikiwa na umeme

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini umetoa kipaumbele kwenye maeneo yanayotoa huduma za kijamii ikiwemo Shule, Taasisi, vituo vya afya, zahanati na maeneo ya visima vya maji kwa sababu ni maeneo yanayotoa huduma kwa jamii.

Kapinga ameyasema hayo leo Machi 18, 2025 katika Vijiji vya Lwangu na Welela vilivyopo katika Halmashauri ya Njombe wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kukagua miradi ya umeme vijijini pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.

“Kipaumbele ni Taasisi kwa sababu zinatoa huduma zinazotunufaisha sisi wote, tunataka umeme ukatumike kwenye vituo vya afya, zahanati, kwenye visima vya maji lakini pia kwenye shule,” amesema.

Ameongeza kuwa, kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini hufanyika tathmini ili kuyabaini maeneo yanayotoa huduma za kijamii huku akibainisha hakuna maeneo yanayo rukwa.

spot_img

Latest articles

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

Waziri Mkuu ataka kazi za Serikali zifanyike Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali inataka kazi zote zifanyike makao...

Mzee Mtei kuzikwa Jumamosi Tengeru

Na Mwandishi Wetu MWASISI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mzee Edwin Mtei anatarajiwa...

More like this