DAWASA YAANZA MSAKO KWA WANAOJIUNGANISHIA MAJI KINYEMELA

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imefanya operesheni katika Mtaa wa Majizzo katika Kata ya Kunduchi Wilaya ya Kinondoni na kubaini matumizi yasiyo halali ya maji yaliyokuwa yakitumika katika shughuli za kilimo cha mbogamboga ambayo imeingiza hasara Mamlaka ya zaidi ya Shilingi Milioni 50.

Mamlaka inaendelea kuchukua hatua dhidi ya maunganisho haramu na kuwaonya wananchi kutumia huduma ya maji kwa kufuata taratibu.

Meneja wa DAWASA Tegeta, Mhandisi Edson Robert amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Mamlaka katika kuhakikisha taratibu za matumizi ya maji zinafatwa kisheria na kuzuia vitendo vinavyoweza kuathidu upatikanaji wa huduma kwa wananchi wengine.

“Operesheni hii imefanyika bada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu matumizi yasiyo ya halali, Natoa rai kwa wafanyabiashara ni vyema kufika katika ofisi zetu na kupata taratibu stahiki badala kuamua kufanya maunganisho kiholela” amesema Mhandisi Edson.

Mjumbe wa Shina namba 5 katika Mtaa wa Majizo Ndugu Jumbe Said amepongeza jitihada za Mamlaka kwa kushirikiana na wananchi katika mapambano dhidi ya upotevu wa maji amesisitiza operesheni hiyo iendelee ili kuwezesha kukamata wahalifu wengine.

“Nawapongeza DAWASA kwa operesheni hii tunaomba adhabu kali itolewe ili iwe funzo kwa wengine na amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa kwani wanaoathirika moja kwa moja na uharibifu wa miundombinu kwa kukosa huduma ni wananchi hivyo utoaji taarifa ni jambo muhimu kwa msingi wa huduma bora” amesema Mjumbe Said.

spot_img

Latest articles

DAWASA YAPELEKA TABASAMU KUNDI MAALUM WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imehitimisha wiki ya...

TANESCO YANG’ARA TUZO ZA UMAHIRI WA MAWASILIANO KWA UMMA

📌 Yanyakua tuzo nne katika vipengele mbalimbali 📌 Yatambuliwa kwa ubora katika mawasiliano ya kimkakati,...

BRELA YAFUNGUA FURSA YA URASIMISHAJI KWA WADAU WA UCHUMI WA UBUNIFU ARUSHA

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka kambi ya...

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM SOMBI ATEMBELEA KIKUNDI CHA UKOMBOZI WA VIJANA KALAMBO

Na Mwandishi Wetu IKIWA ni sehemu ya shughuli za Wiki ya UVCCM 2026, Makamu...

More like this