Vipengele 63 Kuing’arisha The Serengeti Awards 2026

Na Mwandishi Wetu

JUMLA ya vipengele 63 vitaingia katika kinyang’anyiro cha The Serengeti Awards 2026, huku wadau wa uhifadhi na utalii wakipewa fursa ya kuonyesha kazi, ubunifu na mafanikio yao katika sekta hizo.

Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dk. Thereza Mugobi, amesema vipengele hivyo vimegawanyika katika makundi saba ambayo ni People’s Choice Awards, Tourism Operator Awards, Tourism Guide Awards, Best Accommodation and Restaurant Services, Conservation Awards, Tourism Exhibitor Awards na Special Appreciation Awards.

Amesema idadi ya vipengele imeongezeka kutoka 56 mwaka jana hadi 63 mwaka huu baada ya Serikali kupokea maoni kutoka kwa wadau na kufanya maboresho katika mchakato wa tuzo hizo.

Dk. Mugobi amesema Serengeti Awards zinafanyika kwa mara ya pili ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kutambua, kuthamini na kuenzi mchango wa wadau katika uhifadhi wa maliasili na urithi wa Taifa pamoja na uendelezaji wa utalii.

Amesema tuzo hizo pia zinalenga kutoa motisha kwa wadau kuboresha utendaji, kuhamasisha ubunifu na kuongeza ushindani wa Destination Tanzania katika soko la utalii la ndani na kimataifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Serengeti Awards, Hatibu Madudu, amesema ongezeko la vipengele limezingatia maoni ya wadau pamoja na changamoto zilizobainika katika mchakato wa mwaka uliopita.

Amesema wananchi watapata nafasi ya kushiriki katika mchakato wa kuwapata washindi wa baadhi ya vipengele, huku wadau kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiruhusiwa kuwania tuzo hizo iwapo watatimiza vigezo vilivyowekwa.

Dirisha la usajili litafunguliwa Agosti 20, 2026 na kufungwa Septemba 30, 2026, kupitia tovuti rasmi ya tuzo hizo www.serengetiawards.go.tz, ambako wadau watapata taarifa kuhusu vipengele, vigezo na taratibu za kushiriki.

Serikali imewahakikishia wadau kuwa mchakato wa Serengeti Awards 2026 utasimamiwa kwa kuzingatia misingi ya uwazi, usawa na uadilifu ili kuhakikisha washindi wanapatikana kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

More like this

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...