BEKI WA YANGA APANDISHWA CHEO AWA SAJENTI

Na Mwandishi Wetu

Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), kimempandisha cheo mchezaji wetu Ibrahim Hamad “Ibra Bacca” kutoka Koplo na kuwa Sajenti kutokana na kuonesha kiwango bora Uwanjani.

Akizungumza baada ya kupandishwa cheo hicho, amesema anakishukuru kikosi chake kutokana na sapoti wanayoitoa kwake kila sehemu anayopita na kuahidi kuendelea kuitumikia nchi yake.

“Sina budi kushukuru kikosi changu kwa kuweza kunisapoti kwa kila hatua. Nitaendelea kuipambania nchi yangu,” amesema Sajenti Ibrahim Bacca ambaye wazazi wake pia ni askari.

Beki huyo alisajiliwa na Yanga  msimu wa  2022/2023 kutoka KMKM  ambacho ni  kikosi cha ulinzi cha Zanzibar ambacho kina jukumu la kulinda mipaka ya bahari dhidi ya magendo, uvuvi haramu, na vitendo vingine vya kihalifu. Pia, KMKM husaidia katika operesheni za uokoaji baharini na usalama wa majini.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya...

More like this