Mramba: Umeme wa Jotoardhi kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo 2030

📌 *Mikoa 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi

📌 SEforALL yatakiwa kuwekeza katika utafiti na ubunifu

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA imelenga kuunganisha nishati ya jotoardhi kwenye gridi ya taifa ifikapo mwaka 2030 ili kuwa na umeme wa uhakika unaotokana na nishati jadidifu kuelekea Dira ya Tanzania 2025 ambayo inasisitiza maendeleo endelevu ya nishati kama nguzo ya mabadiliko ya kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba katika mjadala wa viongozi wanaoshiriki mkutano wa Kimataifa wa nishati endelevu kwa wote (SEforALL) unaofanyika katika jiji la Bridgetown nchini Barbados.

“Lengo letu ni kuunganisha nishati ya jotoardhi kwenye gridi ya taifa ifikapo 2030, Suala hili ni miongoni mwa azma yetu pana ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa wote ifikapo 2030 ili kuondokana na uzalishaji wa hewa ukaa ifikapo 2050.

“Hii ni kutokana na Sera ya Taifa ya Nishati ya Tanzania 2015 yenye Mpango Mkuu wa Nishati 2020 pamoja na Tamko la Dar es Salaam la “Mission 300” katika Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa 2025”. amesema Mha. Mramba.

Ameongeza kuwa, mikoa 16 nchini Tanzania itanufaika na maendeleo ya nishati ya jotoardhi, na kuifanya kuwa msingi wa mkakati wa nishati endelevu, Nia hii inajidhihirisha kupitia uanzishwaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) kwa lengo la kutafiti na kuendeleza rasilimali za jotoardhi ambapo hadi sasa kampuni hiyo inafanya kazi katika maeneo zaidi ya 50.

Aidha Mha. Mramba, amesema kuwa ili kuvutia uwekezaji, Serikali imeweka mfumo madhubuti wa Sera na udhibiti kuvutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ili kufanya tafiti na kufungua uwezo kamili wa rasilimali hiyo kuwa chachu kwa taifa.

“Kwa kutambua umuhimu wa kimkakati, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipa kipaumbele nishati ya jotoardhi katika ajenda ya kitaifa ya maendeleo ya nishati,” amesema.

Naye, Waziri wa Nishati wa Shirikisho la St. Kitts na Nevis, Konris Maynard amesema kuwa nchi zinatakiwa ziwe tayari kukuza matumizi ya jotoardhi na kuhama katika katika matumizi ya nishati zisizo salama kwa mazingira.

Aidha amewataka wadau walioshiriki mkutano huo kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati ya jotoardhi.Tanzania imebarikiwa kuwa na uwezo mkubwa wa nishati ya jotoardhi, unaokadiriwa kuwa zaidi ya 5,000 MW za umeme na 15,000 MW za nishati ya joto.

Vilevile, Tanzania ina bahati ya kuwa katika eneo la kijiografia ambapo kwa upande Mashariki na Magharibi imezungukwa na Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (EARS), hali hii inaifanya Tanzania kuwa na msingi wa kijiolojia unaofaa kwa ajili ya kutumia rasilimali hiyo Jadidifu.

spot_img

Latest articles

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...

Yanga yatua Zanzibar kuitengenezea dozi AS FAR Rabat

Na Winfrida Mtoi Kikosi cha Yanga kimetua visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya kuikabili AS FAR...

Rais Samia atangaza Baraza Jipya la Mawaziri, nane watemwa

Tatu Mohamed na Winfrida Mtoi RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,...

More like this

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...

Yanga yatua Zanzibar kuitengenezea dozi AS FAR Rabat

Na Winfrida Mtoi Kikosi cha Yanga kimetua visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya kuikabili AS FAR...

Rais Samia atangaza Baraza Jipya la Mawaziri, nane watemwa

Tatu Mohamed na Winfrida Mtoi RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,...