Na Mwandishi Wetu
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe ataendelea kuliongoza shirikisho hilo hadi 2029 baada ya kuchaguliwa katika nafasi katika uchaguzi uliofanyika leo Machi 12,2025, Cairo, Misri.
Motsepe ambaye amekuwa Rais wa shirikisho hilo tangu mwaka 2021, amechaguliwa akiwa ni mgombea pekee katika nafasi hiyo.
Naye Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF), Wallace Karia amechaguliwa mjumbe Kamati ya Utendaji ya (CAF), akiwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kuwakilisha Kanda ya Soka ya Baraza la vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).