Kapinga azindua Namba ya bure ya Huduma kwa Wateja wa Tanesco

📌Awapongeza TANESCO kutekeleza agizo la Mhe. Dkt. Biteko kuwataka kuanzisha namba ya huduma kwa wateja bure

📌Asema namba hii ya 180 ya bure kwa wateja kuimarisha huduma kwa wateja na kutatua changamoto zao

📌Awaagiza Mameneja wa Mikoa na wilaya wa TANESCO kuwasimamia watoa huduma

📌Awaasa watanzania kutumia namba hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga leo Machi 12, 2025 amezindua namba mpya ya huduma kwa wateja (mchongo 180) itakayotumiwa na wateja bure bila malipo ili kupata huduma mbalimbali kupitia kituo cha miito ya simu cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kuanzishwa kwa namba hiyo inafuatia agizo lililotolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko la kuwataka TANESCO kuhakikisha wanakuwa na namba ya bure bila malipo kwa wateja ili kuboresha utoaji huduma kwa wateja na kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima na kuongeza wigo wa wapokeaji wa simu kutoka namba ya awali hadi 150 kwa awamu.

“Naomba niwahakikishie kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusudia watanzania wapate umeme wa uhakika na kuongeza kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kuisimamia TANESCO na taasisi nyingine chini ya Wizara kuhakikisha sekta ndogo ya umeme inakuwa na kuleta maendeleo kwa Watanzania,” amesema.

Awali akizungumza kabla ya mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Balozi Zuhura Bundala amesema mapinduzi kwenye utoaji huduma kwa wateja ni moja ya masuala ya kipaumbele ili kuchochea uchumi wa Nchi na kuongeza kuwa shughuli za uchumi zinategemea sana uwepo wa umeme wa kutosha na uhakika na ndio maana bodi imejipanga kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa na Wizara.

Amesema bodi iko tayari kuhakikisha TANESCO inafanya kazi kwa bidii na jkutoa huduma bora kwa wateja ili kupunguza kero na changamoto za masuala mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mha. Gissima-Nyamo Hanga amesena dunia ya sasa ya biashara na ushibdani wa kibiashara unategemea uwepo wa huduma bora ya uneme na kutatua changamoto kwa wakati.

Aidha, Mha. Gissima amesema licha ya kujipanga kutoa huduma bora kwa wateja pia wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo uhamasishaji wa matumizi bora ya nishati kwa kutumia umeme.Hafla hiyo imehudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati, bodi ya wakurugenzi ya TANESCO na wadau mbalimbali.

spot_img

Latest articles

IST Festival yatumika kunadi mitaji nafuu kwa vijana

Na Mwandishi Wetu TAMASHA la IST Festival lililofanyika jana Februari 14, 2026 kwenye viwanja...

Taliss – IST Swimming Championships yawavuta wenye mahitaji maalumu

Na Winfrida Mtoi MASHINDANO ya mchezo wa kuogelea 'Taliss -IST Championship' yameanza leo Februari 14,...

CRDB na Costech watenga Sh. Bilioni 4.6 kuwezesha mitaji kwa vijana wabunifu

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia TUME ya Sayansi na...

Wanahabari watakiwa kuweka usawa katika uandishi wa mabadiliko ya tabianchi

Na Tatu Mohamed MWAKILISHI wa kimataifa kutoka ActionAid International, Teresa Anderson, amesema ipo haja...

More like this

IST Festival yatumika kunadi mitaji nafuu kwa vijana

Na Mwandishi Wetu TAMASHA la IST Festival lililofanyika jana Februari 14, 2026 kwenye viwanja...

Taliss – IST Swimming Championships yawavuta wenye mahitaji maalumu

Na Winfrida Mtoi MASHINDANO ya mchezo wa kuogelea 'Taliss -IST Championship' yameanza leo Februari 14,...

CRDB na Costech watenga Sh. Bilioni 4.6 kuwezesha mitaji kwa vijana wabunifu

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia TUME ya Sayansi na...