MOIL: Tunaunga mkono kwa vitendo mkakati wa Taifa wa nishati safi

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa MOIL, Altaf Mansoor, ameishukuru Wizara ya Nishati kwa fursa ya kuandaa Kongamano na Maonesho ya Petroli Afrika Mashariki (EAPCE’25), ambalo limefanyika kwa siku tatu.

Akizungumza katika kongamano hilo, Mansoor amesema kuwa limekuwa chachu ya kujifunza mambo mengi muhimu katika sekta ya nishati na limewasaidia kujipanga kwa mustakabali wa kampuni hiyo katika kusaidia juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali kwa ujumla, katika kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia na nishati mbadala kwa ajili ya magari, hususan Gesi Asilia iliyoshindikizwa (CNG).

“Nasi kama MOIL, tunatazama kwa makini fursa hii na tunajipanga kuangalia uwezekano wa kuanza uzalishaji wa nishati hii hapa nchini,” amesema Mansoor.

Kongamano na Maonesho ya Petroli Afrika Mashariki (EAPCE’25) ni jukwaa muhimu linalokutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya nishati kujadili maendeleo na fursa za uwekezaji katika nishati endelevu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

spot_img

Latest articles

Mradi wa Taza kufungua Soko jipya la biashara ya umeme Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mbeya IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya...

Maaskofu, Masheikh nyanda za juu wahimiza uchaguzi wa amani

Na Mwandishi Wetu, Mbeya VIONGOZI wa dini kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamewataka...

SGR yapata ajali, TRC yataja chanzo

Na Mwandishi Wetu Treni ya Mwendokasi (SGR) imeacha njia yake na kupata ajali katika eneo...

More like this