Profesa Mkenda: Miaka 30 ya VETA ni kielelezo cha mafanikio ya Elimu ya Ufundi Stadi nchini

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni kielelezo cha mafanikio makubwa ya serikali katika kuboresha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini.

Ameyasema hayo leo Machi 05, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi nchini na miaka 30 ya VETA.

Amesema kuwa, kwa kipindi cha miongo mitatu, VETA imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwajengea Watanzania uwezo wa kujiajiri, kuajiriwa, na kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi na imekuwa ni taasisi muhimu inayochangia rasilimali watu yenye ujuzi inayohudumu katika sekta mbalimbali, ikiwemo Viwanda, Kilimo, Ujenzi, Teknolojia, Nishati na huduma na Utalii.

“Mwaka huu tunaadhimisha miaka 30 ya VETA ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge mwaka 1994 na kuanza kazi rasmi mwaka 1995. Kabla ya VETA kulikuwa na Idara ya Mafunzo na Majaribio ya Ufundi Stadi (NVTD) katika Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii ambayo ilianzishwa mwaka 1975.

“Maadhimisho haya ni fursa ya kipekee kwa jamii kusherehekea mchango wa ufundi stadi katika maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii, huku tukijipanga kuimarisha sekta ya ufundi stadi ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji ya soko la ajira,” amesema.

Ameeleza kuwa, kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika kuanzia Machi 18 hadi 21 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi huku kauli mbiu ikiwa ni ‘Ukuzaji Stadi na Ubunifu kwa Maendeleo ya Jamii na Taifa’.

Amesema kuwa, shughuli mbalimbali zitafanyika katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho hayo, ikiwemo kutoa huduma kwa jamii, kuendesha maonesho ya ubunifu wa teknolojia pamoja na kutoa tuzo na vyeti vya heshima kwa watu mbambali kwa mchango wao katika shughuli za maendeleo ya Ufundi Stadi nchini.

“Maadhimisho haya ya miaka 50 ya utoaji elimu na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na miaka 30 ya VETA yanakuja wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kukamilishwa ujenzi wa vyuo vya VETA vya hadhi ya kimkoa, katika mikoa yote ambayo haina vyuo vya VETA na vyuo vya VETA vyenye hadhi ya kiwilaya katika wilaya zote ambazo hazina vyuo hivyo.

“Kwahiyo sasa hivi tunakamilisha ujenzi wa chuo chenye hadhi ya Mkoa cha VETA kwa Mkoa wa Songwe na tunaendelea na ujenzi wa vyuo 64 katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazina vyuo hivyo,” amesema na kuongeza:

“Nitumie fursa hii kuwakaribisha katika maadhimisho haya kote nchini yanakoendelea na kipekee katika kilele cha maadhimisho jijini Dar es Salaam ili tukajionee na kujadili umuhimu wa elimu na ujuzi. Kulingana na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023,”.

spot_img

Latest articles

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...

GBT yaikaribisha BetSasa sokoni, yaitaka kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe ameikaribisha...

More like this

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...