Majaliwa: Huduma Jumuishi za kifedha ni kiungo muhimu cha ukuaji uchumi

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa huduma jumuishi za kifedha ni kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Amesema Serikali kwa kutambua hilo imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha sekta ya kifedha inazidi kuwa jumuishi, fanisi, na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.

Amesema hayo leo Machi 3, 2025 alipozindua huduma mpya za kidijitali za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.

Ameongeza kuwa katika vipindi tofauti, Serikali imekuwa ikiandaa na kutekeleza mikakati ya Taifa ya kuboresha huduma jumuishi za kifedha.

“Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023 – 2028 ni mwendelezo wa mafanikio yaliyopatikana kupitia Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha uliokamilika Desemba 2022,” amesema.

Majaliwa ameongeza kuwa jitihada nyingine ni kuandaa Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali wa miaka 10 kuanzia mwaka 2024 hadi 2034.

“Mkakati huu umeainisha malengo mahsusi ambayo kama nchi tunaazimia kuyatekeleza ili kufikia uchumi wa kidijitali,” amesema Majaliwa.

Kwa upande wake, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Sauda Msemo amesema sekta ya fedha imeendelea kuwa na ustahimilivu na hivyo kuwezesha shughuli mbalimbali za kiuchumi kufanyika.

Aidha, Naibu Gavana huyo ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zifuate viwango bora vya usalama wa mitandao na kugundua haraka pale panapotokea udanganyifu wa aina yoyote.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi amesema lengo la uzinduzi wa huduma hizo za NBC kidijitali ni kuboresha utoaji wa huduma za kifedha na kuzifanya zipatikane kwa urahisi.

“Huduma hizo ni pamoja na ufunguaji wa akaunti, kuhamisha fedha, kupata mikopo bila ya kwenda katika tawi,”.

spot_img

Latest articles

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...

Dkt. Biteko: Ufundi Stadi umepewa kipaumbele na serikali

📌 Asisitiza kuwa, Rais Samia anajenga vyuo kila wilaya nchini 📌 Apongeza utoaji wa mafunzo...

More like this