Na Mwandishi Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan amesema anamrudisha Januari Makamba kwa mama kwani alimpiga kofi na kumfichia chakula kama ilivyo desturi ya kina mama pindi mtoto anapomkera.
Rais Samia amezungumza hayo leo Februari 24,2025 wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Lushoto mkoani, Tanga.

“Nataka nimuite mwanangu Januari hapa aje huku,arudi kwa mama, Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kikofi, anakufichia chakula. Sasa mwanangu nilimpiga kikofi na kumfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo,” amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba.

Katika hatua nyingine Rais Samia amezindua jengo la Halmashauri ya Bumbuli, wilayani humo na kusema kuwa madhumuni ya jengo hilo ni kusogeza huduma karibu ambapo na wananchi ambapo huduma zote zitakuwa zinapatikana humo.