Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kenya afariki dunia

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya Wafula Chebukati amefariki Dunia katika hospitali ya Nairobi akiwa na umri wa miaka 62.

Chebukati ambaye alisimamia uchaguzi wa rais wa mwaka wa 2017 na uchaguzi wa wa 2022 ambao uligawanya tume ya uchaguzi alishika hatamu mnamo Januari 2017 kufuatia kuondolewa kwa Ahmed Issack Hassan na makamishna wenzake na kuhitimisha utumishi wake wa miaka 6 kwenye Tume hiyo mnamo Januari 2023.

“Nimepokea habari ya kufariki kwa mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya zamani, Wafula Chebukati kwa masikitiko makubwa. Chebukati alikuwa kiongozi mwenye kanuni na mwenye bidii ambaye aliitumikia taifa kwa uadilifu,” ameandika Rais wa Kenya, William Ruto kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii na kuongeza:

“Kifo chake ni pigo kubwa kwa nchi yetu. Mawazo na sala zetu ziko na familia yake na marafiki wakati huu mgumu. Pumzika kwa amani,”.

spot_img

Latest articles

Yanga yaikung’uta vibaya Mashujaa FC

Na Winfrida Mtoi WANANCHI Yanga wameichakaza timu ya Mashujaa mabao 6-0, huku nyota mpya wa...

Watumishi wapya wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wapigwa msasa

Na Mwandishi Wetu, Pwani OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH), kwa kushirikiana na Chuo cha...

Kituo cha kupoza umeme Mtera kuboresha upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua Kituo cha Kupoza...

Tanesco Kigamboni yatoa elimu y nishati safi ya kupikia shule ya msingi Malaika

Na Mwandishi Wetu KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati...

More like this