Mkesha Maalum wa kuliombea Taifa kufanyika Februari 28, mwaka huu

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka huu, waumini wa Madhehebu mbalimbali nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Mkesha Maalum wa kuombea taifa na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Kanisa la Heavenly Image Manifest, Nabii Edmound Mystic, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkesha Maalum wa kuliombea Taifa utakaofanyika Februari 28, mwaka huu Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu, Watanzania wanatakiwa kuweka kando tofauti za kiimani na kuliombea taifa ili uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani ufanyike kwa amani na ustawi wa maendeleo ya Watanzania wote.

Amesisitiza kuwa kila Mtanzania ana nafasi ya kuombea nchi ipate viongozi waadilifu na wenye hofu ya Mungu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Maombi haya yatawakutanisha viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali, viongozi wa kiserikali na kisiasa…lakini pia kila mtanzania anakaribishwa bila kujali dini yake,” amesema.

Ameongeza kuwa, Kanisa lina nafasi ya kuweza kulibeba taifa kwa namna moja na nyingine kwa kufanya maombi hivyo kupitia maombi hayo yatahusisha pia kumuombea Rais Samia sababu yeye ni mtawala amebeba hatima kubwa ya watanzania.

Amesema hawawezi kuombea serikali wanayoitazamia pasipo kuanza na serikali waliyonayo hivyonni lazima kumuombea Rais Samia ambaye Mungu alimuweka kwenye kiti cha Urais.

“Kuwaombea viongozi wa kitaifa ni jambo nyeti, kwani wao ndio wenye Mamlaka ya kuwaongoza wananchi kuelekea maendeleo wanayokusudia.

“Mungu aliaagiza Februari 28 ni siku ya kutengeneza matokeo ya nchi ya Tanzania bora hivyo kuna umuhimu wa 

Watanzania kusimama na kutengeneza kesho ya nchi yetu kwa maombi. Hatuombei mtu fulani ashinde ila tunaombea yeyote aliyekusudiwa kwa mapenzi ya Mungu kuweza kuchukua kijiti mwaka ujao, bwana awe pamoja nawe,” amesema.

Aidha, amewataka wanasiasa wanaowania nafasi za uongozi kujiepusha na kauli au matendo yanayoweza kuhatarisha usalama wa Taifa.

“Kwa wale wanaogombea nafasi za uongozi, zingatieni haki na sheria zilizowekwa ili yule anayekusudiwa na Mungu aweze kushinda,” amesisitiza Prophet Edmund.

Pia, ameongeza kuwa mazungumzo yenye kujenga amani kati ya vyama vya siasa ni muhimu zaidi kuliko kuhamasisha maandamano yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Mwisho 

spot_img

Latest articles

Viongozi wa dini Kanda ya Magharibi waazimia kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Tabora VIONGOZI wa dini katika mikoa ya Kanda ya Magharibi wameazimia...

Viongozi wa Dini Kanda ya Kusini wataka ulinzi amani, kujitokeza upigaji kura

Na Mwandishi Wetu, Lindi VIONGOZI wa dini mbalimbali kutoka mikoa ya Kanda ya Kusini wamewataka...

Lissu anyimwa dhamana, kesi yaahirishwa hadi Nov 3

Na Mwandishi Wetu Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Mradi wa Taza kufungua Soko jipya la biashara ya umeme Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mbeya IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya...

More like this

Viongozi wa dini Kanda ya Magharibi waazimia kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Tabora VIONGOZI wa dini katika mikoa ya Kanda ya Magharibi wameazimia...

Viongozi wa Dini Kanda ya Kusini wataka ulinzi amani, kujitokeza upigaji kura

Na Mwandishi Wetu, Lindi VIONGOZI wa dini mbalimbali kutoka mikoa ya Kanda ya Kusini wamewataka...

Lissu anyimwa dhamana, kesi yaahirishwa hadi Nov 3

Na Mwandishi Wetu Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...