Wanajeshi 75 wapandishwa kizimbani kwa kukimbia mapigano na M23

Na Mwandishi Wetu

Wanajeshi 75 wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanapandishwa kizimbani leo Februari 10, 2025 wakituhumiwa kukimbia mapigano baina ya vikosi vya Serikali na waasi wa M23.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya Kijeshi wa DRC imeeleza kuwa askari hao pia wanashtakiwa kwa tuhuma za kufanya vurugu dhidi ya raia ikiwa ni pamoja na mauaji na uporaji.

“Wanajeshi 75 wanaokabiliwa na kesi walikamatwa kwa kukimbia mapigano baada ya kushikiliwa kwa Mji wa Nyabibwe. Wanatuhumiwa kwa ubakaji, mauaji, uporaji na uasi,”. imeeleza taarifa hiyo.

Umoja wa Mataifa umeripoti kuwepo kwa vitendo kadhaa vikiwemo ya unyongaji, ubakaji wa magenge na utumwa wa kingono hasa katika eneo la Mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imedai kuwa waasi wa M23 na askari wa Serikali ya DRC pamoja na wanamgambo wanaoiunga mkono Serikali wote wanahusika.

spot_img

Latest articles

TCAA yaimarisha usalama wa anga kwa mifumo ya kisasa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejizatiti kuendana na mabadiliko...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha wadau wa Mahakama

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha...

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

More like this