KAPINGA-KUUNGANISHA UMEME MAENEO YA VIJIJI NI ELFU 27

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema uunganishaji wa umeme kwenye maeneo ya Vijiji ni shilingi 27,000/- na maeneo ya Vijiji mji ni shilingi 320.960/-.

Kapinga ameyasema hayo leo Januari 30, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Bukene, Mhe. Selemani Zedi aliyetaka kufahamu kwa nini maeneo ya Bukene na Itobo hayaunganishiwi umeme kwa gharama ya Shilingi 27,000/-.

“Mheshimiwa Spika maeneo ya Bukene na Itobo ni Vijiji Mji ambapo gharama ya kuunganisha umeme maeneo ya Vijiji Mji ni shilingi 360.960,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuangalia kama kuna uwezekano wa kufanya maboresho kulingana na tathmini amabayo imefanyika.

Aidha, Kapinga amesema tayari amemuagiza Meneja wa Mkoa wa Tabora na wa Wilaya ya Nzega kufanya tathmini ya kina ili yaweze kupatikana majibu ya kina iwapo maeneo ya Bukene na Itobo ili kuweza kuondoa mkanganyiko uliopo.

Akijibu swali Mbunge wa Kilombero, Abubakari Asenga aliyetaka kufahamu kwa nini maeneo ya Katinduka bado yanalipia umeme kwa shilingi 360.960/- wakati ni maeneo ya Vijiji, Kapinga amesema, maeneo ya Vijiji yanaunganishwa kwa shilingi 27,000/- kutokana na Serikali na wafadhili kutoa fedha za kutekeleza miradi ya umeme Vijijini.

Kapinga amesisitiza kuwa sio kila eneo linakidhi vigezo vya kuunganisha umeme kwa shilingi 27,000/-.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Anatropia Theonest, aliyetaka kufahamu ni lini Vijiji vilivyobaki Kyerwa vitafikiwa na huduma ya umeme kikiwepo Vijiji vya Buganza na Nyarigongo, Kapinga amesema maeneo ya Kyerwa umeme umeshafika katika makao Makuu ya Vijiji na kuongeza kuwa Mkandarasi anaendelea na kazi katika kilometa mbili za ziada.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this