Mandonga, Dulla Mbabe wavurugwa, ngumi za aina yake kupigwa Muleba Dec 26

Na Winfrida Mtoi

Mabondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Karim Mandonga na Dulla Mbabe wameahidi kuwapa raha mashabiki wa masubwi Tanzania hasa Kanda ya Ziwa wakati wa mapambano yao ya siku ya Boxing Day iliyopewa jina la ‘Tagi la Mama Samia’ Desemba 26,2024 yatakayofanyika Uwanja wa Zimbihile, Muleba mkoani Kagera.

Katika siku hiyo ambapo mabondia mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watapanda ulingoni, ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Smart Gin ambao ni wadhamini wa pambano hilo yatafanyika pia matukio tofauti tofauti ya burudani.

Kuelekea siku hiyo mabondia hao ni kama wamevurugwa wakitamani tarehe ifike haraka ili kudhihirisha ubabe wao kwa kuwapiga wapinzani wao kwa mara nyingine.Mandonga atachapana na Said Mbelwa, huku Dulla Mbabe akizipiga na mkongwe Mada Maugo.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 5,2024 jijini Dar es Salaam, Mandonga ametamba kuwa atampiga vibaya Mbelwa kuliko amara ya kwanza na safari hii atatumia ngumi aliyoipa jina la Kiberenge, huku Dulla Mbabe akijinadi na mtindo kivita.

Mandonga amesema “Nitaendelea kumpiga Said Mbelwa mimi ndio Mandonga Mtu Kazi akae akijua kipigo kinamhusu sisi ni jiko la shamba halichagui. Mara ya kwanza alishindwa kumaliza raundi na safari hii hatoboi raundi mbili pale Muleba kwa hii ngumi kiberenge,”

“Kifupi tu naweza kusema tunakwenda kwenye vita, yule Maugo anajiita Mbunge wa Rorya sasa nimwambie tu mimi ni Mbunge mtarajiwa wa Kisarawe. Pamoja na kwamba tunakaa wote Chanika siangalii hilo safari hii nitamkanda, mara ya kwanza alijipendekeza nikamvunja kiuno sasa tukutane tarehe 26 mtaona nitakachomfanya,” ametamba Dulla Mbabe.

Akizungumzia sherehe za uzinduzi wa Smart Gin mpya iliyopo kwenye kopo(Ken), Mratibu wa Matukio na Balozi wa kinywaji hicho, Bakari Khatibu amesema siku hiyo kutakuwa na matukio mbalimbali kuhakikisha wale wote watakaofika katika viwanja hivyo wanafurahi.

“Tumekuwa na bidhaa nyingi za Smart Gin lakini safari hii kumekuja na muonekano mwingine mpya, hivyo katika kusheherekea uzinduzi wake tunaanza na tamasha la ngumi la kihistoria pale Muleba mkoani Kagera tukiwa pamoja na PeakTime ambao ni wadau wetu tupo nao kwa muda mrefu,” amesema.

spot_img

Latest articles

Mhudumu wa mochwari mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu wawili akiwamo mhudumu wa mochwari...

Katibu wa fedha UVCCM Dar arudisha fomu ya ridhaa ya ubunge Kawe

Katibu wa Uchumi, Mipango na Fedha UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Ali...

Majaliwa  atangaza hagombei tena ubunge Ruangwa

Na Mwandishi Wetu Waziri mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa leo Julai...

Vijana, Dira na CCM. Chama pekee chenye Imani na vijanaTangu kuasisiwa

Na Mwandishi Wetu TANGU kuasisiwa kwake tarehe 5 Februari 1977 kwa muungano wa TANU...

More like this

Mhudumu wa mochwari mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu wawili akiwamo mhudumu wa mochwari...

Katibu wa fedha UVCCM Dar arudisha fomu ya ridhaa ya ubunge Kawe

Katibu wa Uchumi, Mipango na Fedha UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Ali...

Majaliwa  atangaza hagombei tena ubunge Ruangwa

Na Mwandishi Wetu Waziri mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa leo Julai...