Serikali yawatoa hofu Watanzania kuhusu ubora na usalama wa sukari

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Serikali kupitia Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), imewatoa hofu Watanzania juu ya ubora na usalama wa sukari inayoingizwa nchini kutokana na umakini wa vyombo vyake vya Ulinzi, Usalama pamoja na Mamlaka za Udhibiti kufanya ukaguzi wa sukari yote inayoingizwa nchini kupitia Bandari na mipaka yote nchini ili kuhakikisha usalama wake kwa watumiaji.

Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi, alisema Julai 5, 2024 jijini Dar es Salaam kuwa sukari iliyoingia nchini ina ubora kwa sababu imehakikiwa na Shirika la Viwango nchini (TBS) na kuiruhusu isambazwe kwa walaji.

“Mtu yeyote anayetaka kujiridhisha na ubora na usalama wa sukari iliyoingizwa nchini anaweza kuona nakala za cheti cha ithibati (certificate of conformity) na vipimo vya maabara vya TBS, ukizingatia kuwa kabla ya sukari kuingizwa huwa inakaguliwa vya kutosha nje na mamlaka zinazotambuliwa na TBS,” amesema Profesa Bengesi.

Kutoka hadharani kwa bodi ya Sukari nchini kunatoa majibu halisi na ukweli wa hoja dhaifu zinazotolewa na baadhi ya wadau wa sukari sambamba na kuelezea faida ya mabadiliko ya sheria ya sukari kama mwarobaini wa uhaba wa bidhaa hiyo nchini.

spot_img

Latest articles

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

Viongozi wa dini waendelea kihimiza amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha...

More like this