Uchebe ataja sababu za kurejea Tanzania

Na Winfrida Mtoi

Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Aussems maarufu Ucheba, ametaja sababu ya kurejea kufundisha soka nchini kuwa ni kuvutiwa na mipango ya Singida Black Stars  ambayo amejiunga nayo kwa sasa.

Uchebe ambaye aliipa Simba mafanikio makubwa akichukua mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,  amewasili nchini jana Julai Mosi, 2024 na leo kuzungumza na waandishi wa habari kueleza mikakati yake.

Kocha huyo ameeleza kuwa pamoja na kupata ofa nyingi alizikataa baada ya kupigiwa simu na bosi Singida Black Stars  na kumueleza mipango yao, huku akiahidi kuipaisha timu hiyo hadi kufikia mafanikio kama alivyofanya Simba.

“Unapoitaja Tanzania Ulaya watu wanaijua Simba zaidi. Ikumbukwe wakati naichukua  Simba haikuwa katika hali nzuri  lakini niliitengeneza ikawa timu bora yenye mafanikio, hivyo  ndicho kitu ninachotaka kukifanya Singida na malengo  kwa msimu wa 2024/2025 ni kumaliza nafasi ya tatu,” amesema Uchebe.

Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo, Jonathan Kasano, amesema wana malengo ya muda mrefu na mfupi na ndani ya miaka mitatu wanataka kuwa timu ya ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema wameshafanya usajili kwa asilimia kubwa na walimshirikisha kocha huyo, hivyo ni imani yao watafikia malengo wanahitaji kupitia kocha huyo ambaye ni mzoefu wa kufundisha timu mbalimbali.

spot_img

Latest articles

Yanga yatinga makundi CAFCL kibabe

Na Winfrida Mtoi Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)...

Viongozi wa dini Kanda ya Kati wataka amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma VIONGOZI wa dini mbalimbali kutoka Kanda ya Kati wamewataka Watanzania...

Viongozi wa dini Kanda ya Magharibi waazimia kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Tabora VIONGOZI wa dini katika mikoa ya Kanda ya Magharibi wameazimia...

Viongozi wa Dini Kanda ya Kusini wataka ulinzi amani, kujitokeza upigaji kura

Na Mwandishi Wetu, Lindi VIONGOZI wa dini mbalimbali kutoka mikoa ya Kanda ya Kusini wamewataka...

More like this