Katibu madini, Kamishna wa mafuta, gesi wapewa maagizo

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini na Kamishna wa mafuta na gesi kusimamia mpango wa mafuta na gesi ukamilike kwa haraka na kutumika ili kuendana na mpango wa matumizi bora ya nishati.

Agizo hilo amelitoa leo Alhamisi Mei 30,2024 Jijini hapa wakati wa uzinduzi wa mpango wa matumizi bora ya nishati,pamoja na matumizi ya magari yanayotumia umeme.

Naibu Waziri Mkuu,Biteko amesema mpango wa mafuta na gesi upo katika mchakato wa kukamilika, hivyo viongozi hao wanatakiwa kuharakisha mchakato huo ili uweze kukamilika na kuanza kutumika.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema ni lazima mipango yote isomane ili kusilete sintofahamu yoyote katika utendaji huku akiitaka jamii kuendelea kuungana na Serikali katika juhudi mbalimbali za kutunza mazingira.

“Tuendelee kuungana na Serikali katika juhudi hizi nia yetu baada ya kuzindua kituo hicho tuone vituo vinazinduliwa katika maeneo mbalimbali,huko Mikoani”amesema Naibu Waziri Mkuu Biteko

Biteko amesema amefurahishwa na jinsi ambavyo Jumuiya ya Ulaya na UNDP zinavyoendelea kutoa misaada kwa Tanzania katika miradi mbalimbali.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru kwenye jambo hili kwa kuhakikisha watanzania wanapata nishati bora na yenye gharama ndogo,”amesema Biteko.

Mwakilishi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ,Lamine Dialo amesema Umoja wa Ulaya utaendea kusaidia miradi mbalimbali inayohusu matumizi Bora ya nishati.

Naye,Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Shigeki Komatsubara amesema wataendelea kuhakikisha mazingira yanaendelea kutunzwa nchini kwa kusaidia miradi mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule amemshukuru Naibu Waziri Mkuu kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika kwani kwa Sasa hakuna changamoto yoyote huku akiwakaribisha wadau kutumia jua la Dodoma kuzalisha nishati ya umeme.

spot_img

Latest articles

Mandonga ampa jina jipya Kaoneka, King Class na Nasibu Ramadhani moto utawaka

Na Mwandishi Wetu Kuelekea pambano la ngumi la 'Dar Boxing Derby', bondia Karim Mandonga kama...

FCC yawahamasisha wananchi kulinda Afya na Haki zao dhidi ya Bidhaa Bandia

Na Tatu Mohamed TUME ya Ushindani (FCC) imewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kulinda...

PSPTB yatangaza Mitihani ya 31 ya Kitaaluma, Usajili kufungwa Agosti 15, mwaka huu

Na Tatu Mohamed BODI ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza kuendesha Mitihani ya...

Ewura CCC: Wananchi wadai fidia wanapocheleweshewa kuunganishiwa maji kwa siku saba za kazi

Na Tatu Mohamed BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji...

More like this