Ndoa ya Tanesco na Songas kutamatika Julai mwaka huu

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Serikali imesema kuwa mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na SONGAS utafikia ukomo Julai 31, mwaka huu, na kwamba wameunda timu ya wataalam (Government Negociation Team – GNT) iliyoanza majadiliano mwezi Aprili, 2023 na inatarajia kukamilisha majadiliano hayo kabla ya mkataba kuisha.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma leo Mei 27,2024 na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati akijibu swali la Mbunge, Jesca Kishoa, aliyetaka kujua makubaliano ya mkataba ujao kati ya SONGAS na Serikali yamefikia hatua gani ikiwa mkataba wa awali upo katika mwaka wa mwisho.

Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa Serikali itahakikisha maslahi ya Taifa yanazingatiwa kabla ya makubaliano yatakayofuata.

spot_img

Latest articles

Mufti Zubeir asisitiza upendo, kupuuza wanaoneza chuki za kidini mtandaoni

Na Mwandishi Wetu MUFTI na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally ametoa...

Waziri Gwajima aipongeza Tanesco kuandaa kongamano la wanawake la Nishati Safi ya kupikia

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima...

Makofi, vigelegele vimemrarua Mwigulu Nchemba?

Na Jesse Kwayu KATIKA mfumo wa utawala ambao chimbuko la madaraka ya dola ni wananchi,...

Katibu Mkuu Uwekezaji afanya ziara Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais – Uwekezaji, Dk. Fred Msemwa, leo...

More like this