Safari za ndege Poland hadi Tanzania kuanza

Na Esther Mnyika

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo ya kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Poland hadi Tanzania.

Akizungumza leo Februari 9, 2024 Ikulu, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari baada mazungumzo na Rais wa Poland, Andrzej Duda, Rais Samia amesema ziara ya rais huyo nchini ni fursa ya kuimarisha uhusiano zaidi wa nchi hizo mbili.

Amesema ziara hiyo ni kilelezo kuimarisha uhusiano ulioanza mwaka 1962 ikiwa umetimiza miaka 62.

“Ili kuchochea zaidi utalii na biashara hapa nchini wataalamu wameelekezwa kuchukua hatua zitakazo wezesha kuanza safari za ndege kutoka Poland hadi Tanzania moja kwa moja, tumeweka ombi letu kwa ukubwa nchini Poland, “amesema Dk. Samia.

Amesema Poland ni miongoni mwa nchi 10 ambazo raia wake wengi hutembelea Tanzania kwa shughuli za utalii.

Amesema takwimu zinaonyesha watalii kutoka Poland mwaka 2023 walikuwa 41000 na ndani ya mwezi mmoja mwaka huu wamekuja 6000.

Amesema wamekubaliana na Rais huyo kuimarisha ushirikiano uliopo na kuhamasisha uwekezaji zaidi kwenye sekta za mikakati kama vile viwanda, madini gesi asilia na uchumi wa buluu.

“Tumeendelea uhusiano kati ya Tanzania na Poland katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, elimu, uwekezaji, utalii, viwanda, uchumi wa buluu na TEHAMA,”amesema.

Aidha amewakaribisha wawekezaji hususani wa utalii kuwekeza katika ujenzi hoteli nchini kwa kuwa kuna maeneo mazuri ya uwekezaji katika uzalishaji.

Naye Rais wa Poland, Duda amesema ziara yake nchini imelenga kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na kuleta faida mbeleni.

Amesema wamekuwa na uhusiano wa miaka 62 na Tanzania na kuimarisha uhusiano wao tangu vita ya pili ya dunia.

“Nitaimarisha uhusiano katika sekta ya utalii na watalii kuendelea kuongezeka kuja kutembelea Tanzania na kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania kutoka Poland,”amesema Rais Duda.

Amesema kuimarisha sekta ya elimu, biashara na uchumi ikiwemo wanafunzi kutoka Tanzania kwenda kusoma Poland katika vyuo mbalimbali kwa ufadhili nchi hiyo.

“Vijana watafaidika kusoma katika vyuo hivi watajifunza mambo mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya Tabia Nchi na TEHAMA, watapata ujuzi wa kutunza vitu hivi,”amesema.

Aidha amewalika Rais Dk.Samia nchini Poland ikiwa ni fursa ya kutaanda jukwaa la kuwakutanisha wawekezaji nchini humo kujadili fursa za uwekezaji.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...