Waitara Trophy kutimua vumbi Lugalo

Na Winfrida Mtoi

Shindano la Gofu la kumuenzi aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Mstaafu, George Waitara ‘NBC Waitara Trophy 2024’ litarajia kufanyika Jumamosi Januari 27,2024 ambapo zaidi wachezaji 100 watachuana kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari leo Januari 25,2024 jijini Dar es Salaam, Meneja wa Klabu ya Gofu Lugalo, Kanali David Mzaray amesema shindano hilo ni la wazi kila mtu anaruhusiwa kushiriki.

Amesema katika shindano hilo la kumuenzi muasisi huyo wa Klabu ya Gofu Lugalo, wamealika klabu zote za gofu nchini na hadi kufikia leo wachezaji waliokuwa wamejisajili ni 118.

Ameeleza kuwa idadi hiyo ya wachezaji inatarajiwa kuongezeka kutokana na kasi ya usajili inayoendelea na lengo ni kufikia washiriki 200.

“Shindano hili ni la siku moja na ni la wazi mtu yoyote anaruhusiwa kushiriki kutoka ndani na nje ya nchi. Litashirikisha wachezaji wa division zote, A, B,C, seniors, juniors na ladies na zawani ni kwa washindi wote,”amefafanua Mziray.

Naye Mkuu wa Masoko wa Benki ya NBC ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, David Raymond amesema ni furaha kwao kuona shindano hilo linazidi kukua kila mwaka.

Amesema huu ni mwaka wa nne wanadhamini na wanajivunia kuona mafanikio ya shindano hilo kwani hata wao wana timu inashiriki.

Kwa upande wake Mkuu wa Uhusiano wa SBC, Foti Nyirenda amesema wamedhamini shindano hilo ili kuendeleza ndoto za muasisi huyo klabu ya Lugalo katika kukuza mchezo wa gofu.

spot_img

Latest articles

Hatuna pa kujificha, tuwajibike tu yaishe

TAIFA la Tanzania ni nchi huru iliyojitawala kwa takribani miaka 65 sasa, tangu bendera...

MD TWANGE ATOA RAI KWA MAMENEJA TANESCO KUONGEZA KASI YA KUPAMBANA NA WIZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME

📌Afungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mameneja na Wakurugenzi wa Kanda, Dodoma 📌Asisitiza umuhimu wa...

Yanga yakomaa kileleni, Simba yavizia ikitafuna  miwa Morogoro

Na Mwandishi Wetu WANANCHI Yanga wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu...

WIZARA YA NISHATI YAENDELEA KUTUMIA NISHATI SAFI EXPO KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Nishati inaendelea kutoa elimu ya nishati safi ya kupikia...

More like this