Balozi Nchimbi awafariji Mzee Makamba na Familia ya Mwambi

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kuzungumza na Mzee Yusuf Makamba leo, tarehe 25 Oktoba 2024, jijini Dar es Salaam.

Balozi Nchimbi alifika nyumbani kwa Mzee Makamba, eneo la Wazo Hill, kumfariji kufuatia msiba wa mtoto wake, Sakida Rajab Yusuf Makamba, aliyefariki dunia tarehe 12 Oktoba 2024, mjini Morogoro.

Mzee Makamba, ambaye pia ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, alimshukuru Balozi Nchimbi kwa kufika kumpatia pole na alitumia fursa hiyo kumpongeza pamoja na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwa juhudi zao katika kuimarisha chama.

“Sisi tunawaona, tunawasikia, na tunawafuatilia. Endeleeni kuijenga na kuimarisha CCM. WanaCCM waendelee kufanya kazi ya kujenga na kuimarisha chama kwa bidii zote. Hakuna mwingine atakayefanya kazi hiyo bali wanaCCM wenyewe,” alisema Mzee Makamba.

Mapema kabla, Balozi Nchimbi, akiwa ameambatana na  Issa Gavu, Katibu wa NEC ya CCM Taifa – Oganaizesheni, alifika pia kuifariji familia ya marehemu Balozi Jaka Mwambi, aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu, kufuatia msiba wa mtoto wake, Happiness Jaka Mwambi, aliyefariki dunia Oktoba 24,2024, jijini Dar es Salaam.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...