Ramaphosa aafiki makubaliano ya Israel na Hamas

Johannesburg, Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameafiki makubaliano kati ya Israel na Hamas kuhusu usitishaji wa mapigano kwa siku nne. Usitishaji wa mapigano utakuwa ndani ya saa 24.

Cyril Ramaphosa ni mfuasi mkubwa wa Wapalestina

Kama sehemu ya mpango huo, Hamas itawaachilia huru mateka 50 iliowakamata mwezi uliopita na Israel itawaachilia wafungwa wapatao 150 wa Kipalestina.

Katika taarifa yake, Ramaphosa ameema: “Kama mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa inayotetea amani, haki na utawala wa sheria za kimataifa katika sehemu zote za dunia, Afrika Kusini inaafiki makubaliano yaliyofikiwa.

“Ni matumaini yangu kwamba kufikiwa kwa usitishaji huu wa mapigano kutaimarisha juhudi za kufikia mwisho wa moja kwa moja wa mzozo uliopo,” amesema kiongozi huyo wa Afrika Kusini.

Ikumbukzwe kuwa, Serikali ya Afrika Kusini – inayoongozwa na African National Congress (ANC) – ni mshirika wa muda mrefu wa Wapalestina.

Aidha, imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kutoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ifikapo katikati ya mwezi Disemba kutokana na operesheni ya kijeshi ya Israel katika Gaza.

Ilianzisha operesheni kubwa ya kijeshi mjini Gaza kujibu shambulio la kuvuka mpaka la Hamas Oktoba 7, ambapo watu wasiopungua 1,200 waliuawa na wengine zaidi ya 200 kuchukuliwa mateka.

Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema takriban watu 14,000 wameuawa katika eneo hilo tangu Israel ilipoanzisha kampeni yake ya kulipiza kisasi.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this