PURA yaja na suluhu ya ukosefu wa vyeti vya usalama baharini

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mamlaka ya Udhibiti mkondo wa juu wa petroli (PURA) imebainisha mikakati inayoendelea kutekelezwa ikiwemo kutatua changamoto ya ukosefu wa vyeti vya masuala ya usalama baharini jambo ambalo limekuwa likidumaza ushiriki wa Watanzania katika miradi ya mafuta na gesi asilia.

Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau PURA,Charles Nyangi.

Hayo yamebainishwa Julai 26 Visiwani Zanzibar wakati aikichangia mjadala kuhusu changamoto zinazozuia watanzania wenye ujuzi stahiki kushiriki kikamilifu Katika miradi ya mafuta na gesi asilia kwenye Kongamano la Nishati na Madini na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji wa Wazawa na Uhusishwaji wa Wadau wa Mamlaka hiyo, Charles Nyangi amesema watanzania kushiriki katika miradi ya utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia nchini hususan miradi inayotekelezwa maeneo ya baharini.

Amesema miradi inayotekelezwa nchini na mikakati ambayo PURA inatekeleza kutatua changamoto hizo.

“Akiongelea mkakati wa kutatua moja ya changamoto aliyoitaja kama ukosefu wa vyeti vya masuala ya usalama ili kuweza kufanya kazi maeneo ya baharini, alieleza kuwa PURA iko mbioni kusaini Makubaliano ya Awali na Chuo cha Bahari Dar es Salaam(DMI) kwa lengo la kushirikiana kuanzisha kituo chenye ithibati kinachotambulika duniani kitakachotoa mafunzo hayo nchini,” amesema Nyangi.

Amesema kwa sasa hakuna kituo chenye ithibati nchini Tanzania kinachotoa kozi za masuala ya usalama na tahadhari kama vile Basic Offshore Safety Induction and Emergency Training (BOSIET) yanayowezesha mtu kupata kibali cha kufanya kazi katika miradi ya mafuta na gesi inayotekelezwa baharini.

Nyangi amesema Chagamoto hiyo imepeleka watanzania wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi katika miradi hiyo kulazimika kwenda nje ya nchi kwa gharama kubwa kusomea kozi hizo.

Amesema hiyo ni changamoto kwa kuwa watanzania wachache ndio wanaoweza kumudu gharama za kwenda nje ya nchi kusoma kozi husiki.

Aidha amesema kuanzishwa kwa kituo hicho nchini, kutawezesha watanzania wengi zaidi kupata cheti cha usalama na umahiri baharini hivyo kusaidia ongezeko la watanzania wanaoshiriki katika miradi ya mafuta na gesi asilia hususan miradi ya mkondo wa juu wa petroli inayotekelezwa nchini.

spot_img

Latest articles

Serikali yajipanga kuimarisha utumishi wa umma, kuendeleza mageuzi ya kidigitali

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa...

Bokya amtahadharisha mapema Tyson wa Bongo

Na Winfrida Mtoi Bondia Ismail Khalid maarufu Boyka ametamba kutoa kipigo kikali kwa mpinza wake...

Mwili wa Jenista Mhagama Kuzikwa Jumanne Mbinga, Ruvuma

Na Mwandishi Wetu MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa...

Mradi wa upanuzi Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Kinyerezi I Extension umekamilika

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema kuwa mradi wa upanuzi...

More like this

Serikali yajipanga kuimarisha utumishi wa umma, kuendeleza mageuzi ya kidigitali

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa...

Bokya amtahadharisha mapema Tyson wa Bongo

Na Winfrida Mtoi Bondia Ismail Khalid maarufu Boyka ametamba kutoa kipigo kikali kwa mpinza wake...

Mwili wa Jenista Mhagama Kuzikwa Jumanne Mbinga, Ruvuma

Na Mwandishi Wetu MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa...