JKCI mbioni kuanza kupandikiza moyo

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeeleza kuwa matarajio yaokwa miaka mitano ijayo ni kuanza kupandikiza moyo kwa watu wenye umri mkubwa kwa sababu moyo unakuwa umechoka kufanya kazi.

Akizumgumza Julai 18 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge amesema taasisi hiyo ni hospitali maalumu inayotoa tiba ya magonjwa ya moyo, mafunzo na utafiti.

“Miaka mitano ijayo tunatarajia tuwe tunapandikiza moyo lazima kuwe na maandalizi ya sheria itapitiwa ili watu waweze kujitolea moyo kama mtu amepata ajali uwezekano wa kupona haupo au mgonjwa yupo mahututi hawezi kupona anaweza kusema tuchukue moyo utamsaidia mtu mwenye uhitaji wa moyo kama hauna shida yeyote ili aendelee kuishi,” amesema Dk. Kisenge.

Amesema bado kuna ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa lakini ugonjwa wa moyo unaongezeka kwa kasi na unapelekea watu kupoteza maisha kutokana mfumo wa maisha uliopo.

Amesema unaweza kuepuka magonjwa ya moyo kwa kufanya mazoezi kwa wiki mara tatu na kwa muda wa nusu saa, kuzingatia lishe bora, kuepuka uvutaji sigara na unywaji pombe uliokithiri.

“Kutambua kiwango cha sukari katika mwili wako kutambua msukumo wa damu na kiwango cha mafuta mwilini na kupima afya ya moyo japo mara moja kwa mwaka kunaweza kukusaidia kujua kama una tatizo hili au kama unatatizo kupatiwa matibabu mapema,” amesema Dk. Kisenge.

Amesema katika mwaka wa fedha uliopita 2022 /23 taasisi hiyo ilitengewa bajeti ya Sh bilioni 44.5 zilitumika katika shughuli mbalimbali za sekta ya afya.

Aidha, Dk. Kisenge amesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 taasisi hiyo imetenga bajeti ya kiasi cha Sh bilioni 66.2 fedha hizo zitatumika kwenye utekelezaji wa kazi na mipango mbalimbali.

Ametaja mipango mingine kuwa ni kuimarisha tiba moyo kwa kudhamini masomo ya muda mfupi na mrefu, kununua vifaa tiba vya kisasa zaidi, kuendeleza ujenzi mbalimbali, kutoa huduma za tiba mkoba kwa kuwafuata wananchi waliopo mikoani wanashinda kufika Dar es Salaam.

Ameeleza kuwa manufaa ambayo wananchi watapata kupitia vipaombele vya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha huu ni kukamilika kwa jengo la utawala na vipimo ambali limegharimu kiasi cha Sh bilioni 3.6 .

“Kutasaidia wagonjwa wengi zaidi kupata huduma za vipimo vya moyo kwa wakati pia wafanyakazi watakuwa na ofisi za kutosha na hivyo kupunguza msongamano. Katika ofisi walizopo sasa,” ameeleza Dk. Kisenge.

Amesema kabla taasisi hiyo haijaanzishwa, kwa mwaka wagonjwa walikuwa wanapelekwa kutibiwa nje ya nchi kwa gharama ya Sh bilioni 62.3.

“Tangu taasisi hiyo ianzishwe na uwekezaji wa Serikali kwa mwaka matibabu ya wagonjwa wa moyo yanagharimu Sh bilioni 31 tunaweza kuokoa bilioni 31 zilizokuwa zinapotea kupeleka wagonjwa nje ya nchi,” amesema Dk. Kisenge.

Akizungumzia kuhusu wagonjwa kutoka nje ya nchi amesema kipindi cha mwaka mmoja wagonjwa waliotibiwa katika taasisi hiyo kutoka nje ya nchi walikuwa 301 kupitia wagonjwa hao walipata kiasi cha fedha Sh milioni 200.

Amesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu magonjwa ya moyo kwa kupitia vyombo habari na amewasisitiza waendelea kufanya mazoezi na kufuata lishe bora ni muhimu.

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...